Rais

Denis Becirovic, mjumbe kutoka ofisi ya Rais wa Bosnia na Herzegovina, amempongeza Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, akimwita rafiki wa kweli, huku pia akisisitizia umuhimu wa msaada wa Ankara kwa Sarajevo.

Katika mahojiano yake maalumu na Anadolu, Becirovic alizungumzia uhusiano kati ya Uturuki na Bosnia-Herzegovina akisema kuwa sio wa kisisa na kiuchumi tu lakini uliokita mizizi kwenye kihistoria, utamaduni na mahusiano ya kidini.

Alisema kuwa zinashirikiana katika masuala ya kiusalama, ulinzi na biashara.

Akizungumzia vikao vyake viwili na Erdogan, alisema: Tumekutana mara kadhaa ndani ya miaka miwili iliyopita na kujadiliana masuala mbalimbali. Tumejadiliana namna ya kuimarisha amani na utulivu katika kanda na Bosnia-Herzegovina.”

“Ni jambo la kuridhisha kumuona Rais wa hadhi ya Erdogan, akiiunga mkono Bosnia na Herzegovina. Yeye ni rafiki wa kweli wa Bosnia na Herzegovina, kama anavyojidhihirisha kupitia maneno na matendo. Kwahiyo ni muhimu sana kwa Rais wa Uturuki na nchi yake kuunga mkono mchakato wa amani wa Bosnia-Herzegovina.

Katika masuala ya kiuchumi, Becirovic aligusia mafanikio ya kiuchumi kati ya nchi hizo katika miaka ya hivi karibuni, huku wakiwa wamejiweka lengo la kufikia Dola Bilioni 1 za ujazo wa kibiashara.

Pia alisisitiza kuwa uhusiano wa nchi hizo mbili unaweza kuimarishwa kwenye maeneo mengine kama vile nishati na miondombinu.

Mchakato wa mtangamano kati ya Marekani na Umoja wa Ulaya

Kiongozi huyo alisisitizia nia ya nchi yake kukuza ushirikiano na Washington kufuatia kuapishwa kwa Rais mteule Donald Trump.

“Natumai kuwa sera za Marekani kwa Bosnia na Herzegovina zitabakia vile vile katika siku zijazo.”

Hali kadhalika, aliilaani Serbia kwa kujihusisha na masuala ya ndani ya Bosnia na Herzegovina.

“Tumeshuhudia mateso makubwa kutokana na hili.

“Hata hivyo, ni imani yetu kuwa hatua ya Umoja wa Ulaya itakuwa na manufaa kwa Bosnia na Herzegovina.”

TRT Afrika