Erdogan amesema kuwa Uturuki " itatua suala la wakimbizi kwa kutumia busara zaidi na si hofu." /Picha: AA  

Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan ameelezea wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa matamshi na mashambulizi ya Israeli dhidi ya Lebanon hasa kuhusiana na mustakabali wa eneo hilo.

"Hakuna taifa lolote katika ukanda wetu, ikiwemo Uturuki, itajisikia kuwa salama iwapo uchokozi wa Israeli unaoongozwa na utawala wa Waziri Mkuu wa Israeli,Benjamin Netanyahu hautokomeshwa," alisema Erdogan, baada ya kikao na Baraza la Mawaziri, jijini Ankara siku ya Jumanne.

Hezbollah na Israeli wameendelea kushambuliana mpakani toka kuanza kwa vita vya Gaza mwezi Oktoba mwaka jana, lakini ongezeko la hivi karibuni limezua mtafuruku mkubwa zaidi.

Dhidi ya nia ya kujitenga

Kuhusu sera ya nje ya Uturuki, Erdogan alisema: "Tunaamini kuwa inalipa kuweka mikono wazi kwa sera ya nje. Hatutosita kukutana na yeyote yule aliye tayari kwa jambo hili."

Alisema kuwa Uturuki itaendelea kuhakikisha usalama wa "nchi yetu na watu wetu" ili mradi kuna uwepo wa "vikundi vya kiu ya umwagaji damu" nchini Syria huku bunduki zao zikielekezwa kwake.

"Hatuitolei macho ardhi ya mtu yeyote yule, wala hatuna haja ya utawala wowote ule," alisema na kuongeza kuwa Uturuki inalinda na itaendelea kulinda ardhi yake dhidi ya nia za kujitenga.

"Uturuki si nchi wala haitokuwa taifa lenye kutelekeza marafiki zake," Erdogan alisema.

"Tunafahamu vyema ni nani aliandika mchezo huo uliotengenezwa na mabaki ya shirika la kigaidi linalotaka kujitenga. Si sisi, wala taifa letu, wala ndugu zetu wa Syria watakaoingia katika mtego huu mbaya."

Vurugu dhidi ya wakimbizi wa Syria kwenye mitandao ya kijamii

Erdogan alisisitiza kuwa watu 670,000 wamerejea kwenye makazi kaskazini mwa Syria ambayo yaliondolewa ugaidi na Uturuki na wengine milioni 1 wanatarajiwa kurejea miradi itakapokamilika.

Akizungumzia ghasia na mienendo mibaya ya mitandao ya kijamii baada ya uhalifu wa raia wa Syria katika mji wa Kayseri siku ya Jumapili, Erdogan alisema Uturuki "itasuluhisha suala la wakimbizi sio kwa msingi wa chuki au hofu, lakini kwa mfumo wa busara, wa dhamiri kulingana na hali halisi ya maisha, nchi na uchumi."

"Utulivu wa umma ni mstari mwekundu kwa nchi yetu. Bila kujali kisingizio, hatutavumilia kuvuka au kukiukwa kwa mstari huu," alisema.

"Kama tunavyojua jinsi ya kuvunja mikono michafu inayofikia bendera yetu, tunajua pia jinsi ya kuvunja mikono kuwafikia watu wasio na hatia ambao wamekimbilia katika nchi yetu," rais wa Uturuki alisema.

TRT Afrika