President Erdogan / Photo: AA

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, miongoni mwa mambo yamsingi yaliyo jadiliwa wakati wa kikao hicho ni uvamizi wa vikosi vya usalama vya Israel dhidi ya Masjid al-Aqsa, mashambulizi yao dhidi ya Masjid ya Qibla na uingiliaji wao mkali dhidi ya wale walio katika maeneo matakatifu.

Katika mazungumzo hayo, Rais Erdoğan alieleza kuwa yaliyotokea yanaumiza dhamiri za wanadamu wote sawa na Waislamu.

Pia Erdoğan alisisitiza kwamba haiwezekani wakae kimya mbele ya chokochoko na vitisho dhidi ya mashambulizi katika eneo lenya hadhi na la kiroho Masjid al-Aqsa.

Rais Erdoğan alisema kuwa katika kipindi hiki nyeti ambapo Ramadhani inasadifiana na Pasaka, mvutano unaoendelea Gaza na Lebanon haupaswi kuruhusiwa kuongezeka.

Hundreds of people in the al-Aqsa

Amesisitiza kuwa matukio ya makundi yenye itikadi kali ya Kiyahudi kuuvamia msikiti wa Masjid al-Aqsa imeongeza hisia kali na wasi wasi.

Rais Erdoğan amesisitiza juu ya umuhimu wa kuchukuliwa hatua zinazo hitajika ili Waislamu waweze kutekeleza maombi yao bila matatizo yoyote hasa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu.

Ameeleza kuwa ni muhimu kuzuia matukio ambayo yanarudiwa kila mwezi wa Ramadhani yasiwe hatma ya eneo hilo, Rais

Erdoğan alieleza kuwa wako tayari kufanya juhudi zao ili kupata mzizi wa tatizo na kuchukua hatua ili kujenga haki na amani ya kudumu.

TRT Afrika na mashirika ya habari