Uhispania imemfunga Zambia watu wakitegemea ni mmoja katika ya timu tatu kubwa zitakazoshinda kombe la dunia | Picha: Twitter Football Association of Zambia

Uhispania walichukua udhibiti wa pambano hilo ndani ya dakika 10 za kwanza kupitia mkwaju wa Teresa Abelleira nje kidogo ya eneo la hatari.

Kiungo huyo alichukua mguso mmoja na kujiweka sawa kabla ya kutoa shuti kali kwenye kona ya juu kushoto na kumpiga kipa wa Zambia Eunice Sakala na bumbuwazi akibakia tu kusimama na kutazama.

Hispania iliendelea kutengeneza nafasi na wangeweza kuongoza zaidi baada ya Alexia Putellas aliyeng'aa katika nafasi ya chini kushoto. Nyota huyo wa Barcelona alielea na mpira wa krosi kwa Jennifer Hermoso na kufunga bao lake la 100.

Zambia wamebebeshwa furushi nzito la mabao 10, kufuatia tano walizozawadiwa katika mechi yao ya Ufunguzi na Japan Jumamosi. | Picha: Zambia Association of Football Twitter 

Matokeo hayo yanamaanisha Hispania na Japan zitashiriki katika awamu ya muondoano mjini Perth, huku Zambia ikisindikizana na Costa Rica kuondoka katika michuano hiyo.

"Tumepata pointi nyingine tatu, timu ilianza vizuri. Kufunga mabao matano kwenye Kombe la Dunia, mechi mbili ni neema, [tuna] furaha sana.

Jennifer Hermoso, Mshambuliaji wa La Roja, Uhispania

Kufuatia ushindi wao dhidi ya Costa Rica, hii ni mara ya kwanza kwa Uhispania kushinda zaidi ya mchezo mmoja kwenye fainali za kimataifa.

Zambia wamebebeshwa furushi nzito la mabao 10, kufuatia tano walizozawadiwa katika mechi yao ya Ufunguzi na Japan Jumamosi.

TRT Afrika