Kundi C
Droo ya toleo la nane la Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake U-17 imefanyika huko Santo Domingo, Jamhuri ya Dominika, huku kukiwa na matukio mengi ya kuvutia yaliyoahidiwa katika makundi hayo manne.
Kenya ambao ndio mara ya kwanza kufuzu kombe hili, imejikuta katika kundi moja na mabingwa mara mbili Korea Kaskazini (KDPR) na Mexico, ambao walikuwa wa pili katika shindano la 2018 nchini Uruguay. Wengine ni England.
Kundi gumu C, kwa wadada wetu wanaoshiriki mara ya kwanza katika Kombe la Dunia la Wanawake U17 2024 katika Jamhuri ya Dominika mnamo Oktoba. Lakini #JuniorStarlets wetu watamudu changamoto hii ya kihistoria, bila shaka. Kaende kaende!
Japo Wakenya wanaingia kwa mara ya kwanza katika uga huu, wapinzani wanao tazamiwa kuwa hatari zaidi katika kundi lao ni Korea Kaskazini ambao wana uzoefu wa kushiriki na wa kushinda wakiwa na wanashikilia nafasi moja na Uhispania katika idadi ya vikombe walivyonyakua. Korea Kaskazini walishinda kombe hilo mwaka 2008 na 2016.
England hawana sauti kubwa sana katika shindano hili kwani waliwahi kufika nusu fainali na kushindwa hivyo kuchukua nafasi ya nne mwaka 2008 nchini New Zealand.
Kundi A
Nigeria wamewekwa Kundi A pamoja na wenyeji Jamhuri ya Dominika, ambao pia ni mara yao ya kwanza kushiriki kombe hili.
Dominika wanajipa motisha kutokana na kuwa sekta y amichezo imeimarika katika miaka ya hici karibuni kwani waliwakilishwa kwenye Kombe la Dunia la FIFA U-2 kwa mara ya kwanza mwaka jana, huku kikosi chao Olimpiki cha wanaume kimeandaliwa kwa kampeni yao ya kwanza huko Paris 2024.
Mbali zaidi ambapo Nigeria wamefika katika shindao hili ni nafasi ya tatu mwaka 2022 walipofuzu nusu fainali.
Nigeria watapambana katika kundi hili na New Zealand ambao pia mwisho wao uliwahi kuwa nusu fainali 2018.
Pia Ecuador wako katika kundi A.
Kundi D
Zambia, timu ya tatu kufuzu kutoka Afrika wameorodheshwa katika Kundi D pamoja na Japan, Poland na Brazil.
Hii ni mara ya pili kwa Zambia kushiriki shindano hili baada ya kuchujwa hatua ya makundi mwaka 2014 nchini Costa Rica.
Hatari zaidi katika kunid lao ni Japan ambao wamewahi kushiriki mara tatu na kuibuka na ushindi mara moja, mwaka huo huo ambao Zambia waliwahi kufuzu 2014.
Kundi B
Kundi gumu zaidi katika droo hii ni Kundi B iliyojumuisha timu ambazo wote wameshiriki na kufika analau robo fainali katika shindano hili na zaidi.
Uhispania, ambao ndio mabingwa watetezi wameshikilia rekodi ya ushindi mara nyingi, baada ya kushinda mara mbili mtawalia 2018 na 2022.
Pia, tangu 2010, Uhispania hawajawahi kukosa kufika nusu fainali katika kombe hili.
Watakutana na wapinzani wao waliowalaza katika fainali zilizopita, Colombia katika kundi hili
Wengine ambao sio wachache pia ni Korea Kusini kwani wamewahi kushind akombe hili 2010.
Timu inayotamatisha 16 katika shindano hili ni Marekani ambao pia wamo katika Kundi A , wao wakiwa na historia ya kufika fainali mwaka 2008 walipolazwa 2-1 na Korea Kaskazini katika Uga wa New Zealand.
Kombe la dunia la FIFA kwa wanawake wasiozidi miaka 17 litachezwa kuanzia Oktoba 16-Novemba 3 mwaka huu nchini Dominican Republic.