Wenyeji Morocco, wanaoandaa fainali hizo, walikuwa wa kwanza kufuzu kwenye hatua ya fainali walipoifunga Mali 4-3 kupitia njia ya penalti.
Morocco iliifanikiwa kuifunga Mali kwa njia za penalti baada ya kutoka sare ya 2-2 katika muda wa kawaida katika mechi iliyopepetwa katika uwanja wa Prince Moulay Abdellah ulioko mji mkuu wa Rabat.
Kwenye fainali nyingine, Mabingwa watetezi Misri walishinda 1-0 dhidi ya Guinea kupitia bao la Mohamed Shehata Mahmoud huku wakilenga kulihifadhi taji lao. Misri sasa itachuana na Morocco kwenye fainali itakayopigwa mjini Rabat siku ya Jumamosi.
Aidha, Guinea na Mali zitawania nafasi ya tatu mjini Tangier huku mshindi wa mechi hiyo pia akijaza nafasi ya mwisho ya kushiriki kwenye mashindano ya Olimpiki yatakayoanza mwaka ujao.