Luteni-kanali Paul Henri Sandaogo Damiba alitumikia kiasi cha miezi nane kama kiongozi wa Burkina Faso. Aliingia madarakani kwa mapinduzi dhidi ya Rais Roch Marc Kabore Januari 24, 2022, nae akatolewa madarakani Oktoba 2, kupitia mapinduzi makali ya Kapteni Ibrahim Traore.
Mapinduzi mawili chini ya mwaka mmoja! Maraisi--kumi-- wengi wa kijeshi-- katika miaka 62 ya uhuru! Kwa uchache ni kwamba Burkina ina shida kuu ya ustawi wa nchi kisiasa. Hali hii inaweza kuelezeka vipi?
Ugaidi na dosari za Jeshi.
Huenda ukajiuliza iwapo sababu husika hutoa matokeo sawa katika nchi ya Burkina Faso.
Kwa kutetea mapinduzi ya Januari 24, 2022, dhidi ya Roch Marc Christian Kabore, ambaye alichaguliwa Kidemokrasia kwa muhula wa miaka tano, Luteni Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba alidai kwamba kutoweza kwa Rais kudhibiti mashambulizi ya makundi ya kigaidi kutoka Mali.
Hii ikiwa sababu sawia ambayo aliyonadi Kapteni Ibrahim Traore kutetea mapinduzi ya Oktoba 2, 2022.
Hoja inayokataliwa na Mwanahabari na mwandishi wa Burkinabe Lamine Nourridine Konkobo, ambaye huandikia Jarida la pseudonym Aquino d'Sassa, anasema, “Roch Marc Christian Kabore, Rais aliyechaguliwa, alitofautiana na ujuzi wa Jeshi lake katika kutekeleza mikakati dhidi ya magaidi.”
“Kwa hakika jeshi-- ambalo lilifeli vita dhidi ya magaidi-- sasa linajipiga kifua kua mtatuzi wa kupambana na kundi hilo hilo la magaidi kwa kunyakua hatamu ya urais ambayo ni tendo la kushangaza.”
Mazingatio kuu ni kwamba, kuna mambo yanayo zorotesha uwezo wa kudhibiti maadui katika jeshi la Burkinabe. Rais wa zamani Marc Christian Kabore aliunda kamati kubaini vurugu la Inata, ambapo wanajeshi 50 waliuwawa katika shambulio la kigaidi mnamo Novemba 14,2021. Ripoti ya mwisho ilinuia kugusia mapungufu katika jeshi wanapokabiliana na magaidi.
Kwa masikitiko, mapinduzi ya Januari 24 yalizika ripoti hiyo ilisubiriwa kwa hamu na umma ambayo ingedhihirisha aibu za kijeshi.
Licha ya hayo, watazamaji wa siasa za Burkinabe wananakili “Ukosefu wa miundo msingi: vifaa hewa na gari za kujilinda na mashambulizi.”
Vilevile, mwanahabari wa Burkinabe katika jiji la Ouagadougou (amabye tutampa jina la ‘Jules’ kulinda maisha yake) alisema kwamba, “Jeshi limegawanyika kitabaka. Maafisa wa kuu na walioko chini hawana uwiano mwema.”
Ikumbukwe kwamba, kupinduliwa kwa Rais wa zamani Blaise Compaore, ambaye alipundiliwa mwaka wa 2014, ulisababisha udhaifu na kusambatisha ulinzi wa nchi. “Ulinzi wa nchi ulikua umetengewa kulinda mamlaka ili kuhifadhi uongozi. Haikuundwa kulinda wananchi,” Jules anasema. Hii ina maanisha kwamba jeshi, ambalo linafaa kudhihirisha uzalendo, linaafikia siasa duni ya kuhujumu nchi…
Mashirika madogo katika uongozi wa watu
“Katika na sheria hazina mchango; ufisadi, chuki na ushawishi wa mafanikio madogo uezagaa katika umma,” ananakili Lamine Nourridine Konkobo. Katika nchi ya Burkina Faso, kuna takriban mapote matatu: mashabiki wa Compaore, mashabiki wa Rais alopinduliwa Kabore ‘People's Movement for Progress’, na wale wanaohoji kwamba wakipinduzi ni watetezi. Kila pote inatamani mabaya kwa pote lengine inapofika zamu ya kundi kudhiti Ikilu ya Kosyam. Ufidhuli, ujeuri na hasira amabzo zinachochea vurugo ndio maadili siku hizi-- Paul-Henri Damiba alijua hii kinaga ubaga.
Makosa makubwa zaidi ya Paul-Henri Damiba.
Paul-Henri Damiba alipata uongozi kwa urahisi sana kwa ahadi za kudhibiti tishio la kigaidi.
Kwa ushauri wa wanasias fulani, alikiuka ahadi zake. “ Tuliona akiweka kipaumbele kuratibisha uongozi, uwiano wa watu wa Burkinabe,” Ateta Jules.
“Alifungia mchango wa mawazo na kukataa kusikiliza wenzake ambapo usalama umekua donda sugu. Kuingia madarakani kwa Damiba hakukuzuia uvamizi wa magaidi. Magaidi sasa wanamiliki asilimia 40 sehemu ya nchi-- miji kama Nouna, Solenzo na Goro imenyakuliwa.”
Hii ni hali iliyoghadhibisha baadhi ya wanajeshi kama kapteni Ibrahim Traore, aliyetaka kukutana na kiongozi wa nchi-- bila kufaulu!
Licha ya hayo, wa Burkinabe wengi--ikiwemo walioko katika jeshi--hawakuridhia mapokezi ya Blaise Compaore, Rais wa zamani wa Burkina, aliyefukuzwa katika mapinduzi, na sasa ni mkimbizi nchi ya Ivory Coast. Alihukumiwa kifungo cha maisha Aprili 6, 2022, kwa mchango wake katika mauaji ya Thomas Sankara Oktoba 15, 1987, na wengi kunadi ziara yake kuwa “msamaha usiopingika,” “Najisi kwa kumbukumbu za Sankara,” na “kibaba cha kuepuka adhabu.”
Hivyo basi, ushauri kutoka kwa mwandishi Equiano d'Sassa kwa kigogo wa zamani wa Burkina faso: “Kuchukua njia iliyopotea sio rahisi kukwepa.”
Burkina Faso inahitaji usiadizi wa “ECOWAS” ili kuweza kuimarisha mashirika thabiti; inahitaji jamii ya kimataifa kuwekeza katika jeshi lake; na vilevile, inahitaji kupasha habari wananchi.
“Mmoja hawezi ongoza au kuendeleza nchi kwa misururu ya mapinduzi: kinacho hitajika ni katiba inayo heshimika na wote, jeshi la nchi linalolinda nchi na mashirika, na uhuru wa utendakazi. Kwa sababu, hali yetu ni taswira ya akili jumlishi inayohitaji mageuzi,” Atamatisha Equiano d'Sassa.