9 kati ya 10 wanaoanza uvutaji sigara wanaanzia mashuleni / Picha: AP

Shirika la Afya duniani WHO, limetoa wito kwa mataifa ya dunia kuweka marufuku ya pamoja dhidi ya uuzaji au utumiaji wowote wa bidhaa za sigara na nikotini ndani na karibu na mashule.

Hii ni kutokana na takwimu za kutia hofu zinazoonyesha kuwa idadi kubwa ya wavutaji sigara wanaanzia tangu umri wa kwenda shule.

Shirika hilo limeshutumu kampuni za kutengeneza sigara na bidhaa zingine za nikotini kwa kuwalenga vijana katika mauzo.

"Imma iwe darasani, kucheza michezo nje au kusubiri kwenye kituo cha basi lazima tuwalinde vijana dhidi ya moshi mbaya ya sigara na sumu ya sigara ya kielektroniki pamoja na matangazo yanayotangaza bidhaa hizi," Dk Ruediger Krech, Mkurugenzi wa Ukuzaji wa Afya, Shirika la Afya Duniani.

Sasa WHO imetoa mwelekezo mpya, “Ukombozi dhidi ya tumbaku na nikotini: mwongozo kwa shule,” na “mfumo wa zana za shule zisizo na nikotini na tumbaku” ili kusaidia kulinda afya ya watoto kwa wakati ufaao kwa msimu wa kurudi shuleni katika nchi nyingi.

Shirika hilo la afya limesema sekta ya tumbaku inawalenga vijana kwa mauzo ya tumbaku na bidhaa za nikotini na kusababisha matumizi ya sigara za kielektroniki kuongezeka ambapo wavutaji 9 kati ya 10 wanaoanza kabla ya umri wa miaka 18.

''Bidhaa pia zimefanywa kuwa nafuu kwa vijana kupitia uuzaji wa sigara za matumizi moja moja na sigara za kielektroniki, ambazo kwa kawaida hazina maonyo ya kiafya,''amesema Dkt. Ruediger

Hata hivyo shirika hilo limesema kuwa ili muongozo huo uwe na tija, unahitaji inahitaji mbinu ya "shule nzima" - ambayo inajumuisha walimu, wafanyakazi, wanafunzi na wazazi. Ndani yake pia kuna zana za utendaji zinazohamasisha kuhusu jinsi ya kusaidia wanafunzi kuacha uraibu, kampeni za elimu, uundaji wa sera na jinsi ya kuzitekeleza.

TRT Afrika