Na Kevin Philips Momanyi
TRT Afrika, Istanbul, Uturuki
Chuo Kikuu cha Kenyatta nchini Kenya kinaomboleza vifo vya wanafunzi 11 waliofariki katika ajali iliyohusisha basi la Chuo na gari ya mizigo katika barabara kuu ya Nairobi kuelekea Mombasa.
Wanafunzi hao walikuwa katika safari ya masomo kuelekea mji wa pwani ya nchi hiyo Mombasa.
Basi hiyo ilikuwa imebeba jumla ya wanafunzi 58, akiwemo mlinzi mmoja, wakati ilipogongwa upande wa kushoto.
Taarifa zinasema, punde tu baada ya ajali, wanafunzi kumi walipoteza maisha hapo hapo, huku mmoja akifariki wakati wa kupewa matibabu katika Hospitali ya Rufaa iliyopo mjini Voi, Taifa Taveta.
TRT Afrika