Benjamin Zalman Polun, Marcel Malanga na Tyler Thompson, raia wa Marekani wanaoshukiwa pamoja na kundi la watu wengine karibu hamsini kuhusika na jaribio la mapinduzi nchini Congo / Picha : Reuters 

Wakili wa Wamarekani watatu waliohukumiwa kifo nchini Congo kwa tuhuma za kushiriki katika jaribio la mapinduzi aliwasilisha rufaa Jumanne.

Mahakama ya kijeshi nchini Congo ilitoa hukumu ya kifo Ijumaa iliyopita kwa watu 37, wakiwemo vijana watatu wa Marekani, baada ya kuwatia hatiani kwa tuhuma za kushiriki katika jaribio la mapinduzi.

Washtakiwa hao, wengi wao wakiwa ni Wakongomani lakini pia Mwingereza, Mbelgiji na Kanada, walikuwa na siku tano za kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo kwa tuhuma zinazojumuisha jaribio la mapinduzi, ugaidi na kujiunga na chama cha uhalifu. Watu kumi na wanne waliachiliwa huru katika kesi hiyo.

''Congo ni mwanachama wa Mkataba wa Roma, na kwa sababu hiyo kurejeshwa kwa hukumu ya kifo ilikuwa kinyume cha sheria,'' alisema Richard Bondo, wakili wa Wamarekani waliohukumiwa. ''Bunge lilipaswa kuamua juu ya adhabu mbadala, Bondo aliiambia AP - lakini haijafanya hivyo hadi sasa,'' aliongeza Bondo.

DRC ilirudisha hukumu ya kifo mapema mwaka huu, na kuondoa usitishaji uliodumu kwa zaidi ya miongo miwili, huku mamlaka ikijitahidi kuzuia ghasia na mashambulizi ya wanamgambo nchini humo. Wanaume waliopatikana na hatia katika jaribio la mapinduzi wanaweza kuuawa kwa kupigwa risasi.

Malanga aliuawa kwa kupigwa risasi akipinga kukamatwa mara tu baada ya kutiririsha moja kwa moja shambulio hilo kwenye mtandao wake wa kijamii, jeshi la Congo lilisema.

Mtoto wa kiume wa Malanga, Marcel Malanga, mwenye umri wa miaka 21, ambaye ni raia wa Marekani, na Wamarekani wengine wawili walihukumiwa katika jaribio hilo la mapinduzi.

TRT Afrika
AP