Wakimbizi kutoka Sudan waongezeka huku UNHCR ikisimamisha shughuli katika maeneo kadhaa

Wakimbizi kutoka Sudan waongezeka huku UNHCR ikisimamisha shughuli katika maeneo kadhaa

Ndani ya Sudan kwenyewe , wakimbizi pia wamelazimika kuhama katika makambi yao
Ethiopia, Chad, Misri, Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati zinapokea wakimbizi kutoka Sudan   / Photo: AA

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi , UNHCR linasema tangu mapigano kati ya jeshi la Sudan na vikosi vya Rapid Support Forces kuanza tarehe 15 Aprili, zaidi ya watu 50,000 wameikimbia Sudan.

Chad, Misri, Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati zinaendelea kupokea wakimbizi kutoka Sudan.

"Nchini Misri, Serikali imeripoti kupokea watu 16,000, ambapo 14,000 ni wa asili ya Sudan,” UNHCR inasema kwa taarifa.

Nchini Chad wakimbizi 7,500 kati ya angalau 20,000 ambao wamevuka mpaka katika wiki moja iliyopita au zaidi wamethibitishwa.

Takriban watu 14,000, hasa raia wa Sudan Kusini wanaorejea nchini kwao wamekimbilia Sudan Kusini.

Katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na Ethiopia takwimu kamili bado hazijabainishwa, lakini shirika hilo linasema idadi ndogo ya waliofika imebainika.

Ndani ya Sudan kwenyewe , wakimbizi pia wamelazimika kuhama,

“Tumepokea ripoti kwamba karibu wakimbizi 33,000 wamekimbia kutoka Khartoum kutafuta usalama katika kambi za wakimbizi katika jimbo la White Nile, 2,000 kwenye kambi za Gedaref, na 5,000 hadi Kassala, tangu mgogoro ulipoanza wiki mbili zilizopita, kwa mara nyingine tena wakikimbia kuokoa maisha yao. ,” UNHCR inasema.

TRT Afrika