Jenerali Abdourahamane Tchiani kiongozi wa kijeshi Niger ametangaza baraza mpya ya mawaziri / Picha: Reuters

Utawala wa kijeshi wa Niger umetangaza serikali mpya yenye mawaziri 21 katika agizo lililosomwa kwenye televisheni ya taifa.

Inakuja kabla ya mkutano wa dharura wa viongozi wa jumuiya ya Afrika Magharibi ECOWAS kuhusu mapinduzi nchini Niger, baada ya wakuu wa jeshi la nchi hiyo kukaidi makataa ya kumrejesha rais aliyechaguliwa.

Serikali mpya ya Niger ilitangazwa na Jenerali Abdourahamane Tchiani, ambaye alisoma taarifa yake Jumatano usiku.

Waziri Mkuu Ali Mahaman Lamine Zeine ataongoza utawala huo wenye wanachama 21, huku majenerali kutoka baraza jipya la uongozi wa kijeshi wakiongoza wizara ya ulinzi na mambo ya ndani.

Serikali ya mpito kuteuliwa kwa waziri mkuu mpya na viongozi wa mapinduzi mapema wiki hii kulionekana kuashiria kuanza kwa mpito kwa serikali mpya.

Wiki mbili baada ya mapinduzi yaliyomwondoa madarakani Mohamed Bazoum, ECOWAS inasema inatafuta suluhu la kidiplomasia lakini haijaondoa kutumia nguvu kutatua mgogoro huo.

Maamuzi muhimu yanatarajiwa kutoka kwa mkutano katika mji mkuu wa Nigeria Abuja, kulingana na taarifa kutoka kwa shirika hilo lenye mataifa 15 siku ya Jumanne.

TRT Afrika