Celik amesema Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan atatangaza "siku tatu za taifa kuomboleza" baada ya mashambulizi ya Israel katika hospitali kuuwa zaidi ya watu 500./Picha: AA

Msemaji wa Chama cha AK Omer Celik amesema kwamba mashambulizi ya Israel dhidi ya Palestine ni “moja ya mauaji ya halaiki yaliyopangwa katika historia ya sasa.”

Kauli yake imetolewa katika mkutano wa waandishi habari siku ya Jumatano, siku moja tu baada ya zaidi ya watu 500 kuawa katika shambulizi la anga la Israel katika hospitali ya Al Ahli Baptist iliyopo Gaza.

"Israel inawanyima haki ya kuishi Wapalestina katika ardhi yake na kuwashambulia kwa mabomu. Israel imewaambia hawa watu (Wapalestina) kuondoka katika makazi yao na kwenda kusini halafu inawapiga mabomu wakati wakikimbia," Celik amesema.

"Hatimae, watu wamekimbia katika hospitali, wakidhani kuwa huenda Israel haitashambulia, lakini Israel imewapiga mabomu wakiwa katika hospitali," ameongeza.

"Haya ni mauaji ya halaiki kuwahi kushuhudiwa katika historia ya binadamu."

Msemaji huyo amesisitiza kwamba, Uturuki inalaami “ukatili huu kwa aina yote.”

Celik pia amesisitiza kwamba, Uturuki inasimama pamoja na watoto waliodhulumiwa, wanawake, wazee, na wananchi wa Palestina.

“Mateso ya Palestine ni mateso yetu, na madhara haya ni mathara kwa jamii yote."

'Ukatili ya Israel wa kupitiliza'

"Kushambulia hospitali ambapo kuna wanawake, watoto, na raia wasiokuwa na hatia na katika mashambulizi ya Israel ya hivi karibuni ambayo yamekiuka misingi ya kibinadamu," rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema katika mtandao wa X.

"Naiomba jamii kuchukua hatua kusitisha ukatili wa hali ya juu wa Israel katika eneo la Gaza,”ameongeza.

Picha zimeonyesha maiti zilizotawanyika katika uwanja wa hospitali.

Maelfu ya Wapalestina walikuwa katika hospitali pindi jengo liliposhambuliwa kwa bomu.

Israel imekataa kuhusika kwa shambulio hilo la anga, huku jamii ya kimataifa ikitaka kufanyike kwa uchunguzi ili kuthibitisha nani alihusika.

Shambulio hilo la anga, limetokea siku ya 12 tangu vita kati ya Israel na Hamas kuanza, huku kukiwa na kilio kutoka jumuia ya kimataifa na mashirika na viongozi wa dunia wakisema mashambulizi ya mabomu ya Israel katika eneo la Gaza ikiwemo vituo vya afya, makazi, na sehemu za kufanyia ibada ni ukiokaji wa sheria za kimataifa na inaweza kupelekea uhalifu wa kivita.

TRT Afrika