Uwezo wa Sudan kuendelea kuwa muuzaji mkubwa wa ubani unaendelea kudidimia kutokana na vita vilivyoanza Aprili 2023 / Picha: Reuters

Na Coletta Wanjohi

Istanbul, Uturuki

Afrika ndiyo mzalishaji mkuu duniani wa ubani au gum. Ubani Arabic au gum Arabic unatokana na aina fulani za miti ya mgunga au acacia tree.

Miti ya mgunga hutoa utomvu baada ya kukatwa chale kwenye magome yake ambayo huruhusu kioevu kutoka nje.Baada ya hayo, majimaji hayo au sap hugeuka kuwa ubani au gum.

Ubani Arabic au gum Arabic unatokana na aina fulani za miti ya mgunga au acacia tree/ Picha: AFP 

Lakini Sudan ndiye mzalishaji mkubwa na vile vile mdau mkuu katika usindikaji na usafirishaji wa ubani kwenye masoko duniani kote.

Umuhimu wa ubani au gum Arabic ni nini?

-Katika sekta ya chakula na vinywaji, ubani hutumika kama kiimarishaji. Unatumika mara kwa mara ili kuboresha umbile na midomo, na kuepuka ukaushaji katika vyakula vilivyochakatwa, vinywaji baridi na vile vilivyookwa.

• Katika dawa, hutumika kufunika vidonge, kutengeneza dawa za maji na kuunganisha vidonge

Katika dawa, hutumika kufunika vidonge, kutengeneza dawa za maji na kuunganisha vidonge.

Katika nguo hutumika kufanya rangi ibaki kabisa wakati wa uchapishaji wa nguo na kuongeza rangi au dyeing

Katika upigaji picha na uchoraji hutumika kama mipako kwa vitu visivyoweza kuguswa na mwanga na pia kama kiunganishi cha rangi.

Ubani ni bidhaa kuu ya kilimo nchini Sudan baada ya mbegu za mafuta/ Picha: AFP 

Mnamo mwaka wa 2019, Sudan iliuza nje kiasi cha kila milioni 51, 060, 900 cha ubani kwa jumuiya ya Ulaya (51,060,900kg), India kilo 13,414,300, na Uingereza kila 3,299,710kg.

Ubani ni bidhaa kuu ya kilimo nchini Sudan baada ya mbegu za mafuta. Karibu nusu ya uzalishaji wa Sudan (49.3%) unatoka eneo la Kordofan na kuzalishwa katika maeneo megin ya mikoa ya Kassala, Darfur na White na Blue Nile.

Katika Afrika Mashariki, unazalishwa nchini Kenya, Somalia na Tanzania/ Picha: AFP 

Mbali na Sudan, Ubani huzalishwa hasa katika eneo la Sahel barani Afrika, eneo linaloanzia Senegal kwenye pwani ya Atlantiki, kupitia sehemu za Mauritania, Mali, Burkina Faso, Niger,Nigeria, na Chad hadi Eritrea kwenye pwani ya Bahari Nyekundu.

Katika Afrika Mashariki, unazalishwa nchini Kenya, Somalia na Tanzania. Chad ni msafirishaji wa pili muhimu wa gum arabic, baada ya kuizidi Nigeria kwa miaka mingi kati ya 1998 na 2016.

Eneo la Sahel ni kavu na nusu kame, bora kabisa kwa mimea ya mshita.Kwa kuongezea, hali ya hewa ya Sahel ni nzuri kwa uvunaji wa utomvu.

Wakati wa msimu wa uvunaji wa utomvu, halijoto ya juu, unyevunyevu mdogo na mvua kidogo hufanya utomvu kukauka na kuwa mgumu haraka mara tu unapotoka kukatwa kwenye gome la mti.Kisha huvunwa.

Hata hivyo, uwezo wa Sudan kuendelea kuwa muuzaji mkubwa wa ubani unaendelea kudidimia kutokana na vita vilivyoanza Aprili 2023 na kuathiri maeneo ambayo yana kiwango kikubwa cha uzalishaji wa ubani.

Lakini bado Afrika ina fursa kubwa ya kuendeleza biashara hii, kwani huenda ikawa fursa ya nchi nyengine kuzalisha zaidi sasa.

TRT Afrika