Serikali ya Kenya imefanya mkutano na viongozi wa akaunti 47 za Kenya kujadili maendeleo ya ugatuzi/ Picha: Ikulu ya Kenya 

Mnamo 2010, Wakenya walipitisha katiba mpya, ambayo ilianzisha mfumo wa serikali ya ugatuzi yenye serikali 47 za ngazi ya chini.

Utafiti uliofanywa na shirika la Twaweza, ambao ni asasi ya kiraia, unaonesha kuwa Wakenya wanasema kuwa ufisadi na matumizi mabaya ya fedha ni changamoto kubwa za ugatuzi.

"Pia wananchi tuliowahoji walichangia kuwa matumizi mabaya ya fedha, kukosa fedha za kutosha na wananchi kutohusishwa katika uongozi ni changamoto ya kufanya ugatuzi kutofanikiwa," ripoti ya Twaweza inasema.

Maswala haya ndiyo yamekuwa yakijadiliwa katika mkutano wa kitaifa kujadili maendeleo ya ugatuzi. Umehudhuriwa na magavana wa kaunti zote 47 nchini Kenya.

"Pia wananchi tuliowahoji walichangia kuwa matumizi mabaya ya fedha, kukosa fedha za kutosha na wananchi kutohusishwa katika uongozi ni changamoto ya kufanya ugatuzi kutofanikiwa," ripoti ya Twaweza inasema.

Twaweza, Ripoti ya Ugatuzi 2023

Rais William Ruto ameambia viongozi hawa hawa kuwa bado kuna imani kuwa ugatuzi wa huduma za serikali itawainua wananchi.

"Matarajio ya Wakenya kutawala hatima yao na kujiletea maendeleo, yako hai leo kwa sababu ya ugatuzi. Watu wa tabaka jipya la kati wanaongezeka katika vijiji kote Kenya kutokana na ugatuzi,: rais alisema katika mkutano wa taifa wa ugatuzi.

Anakubali kuwa ugatuzi unaathiriwa pakubwa na ufisadi.

"Nimesema wazi kuwa hatutaunga mkono ufisadi, nia ya Wakenya walipokubali kufanya ugatuzi haikuwa kufanya ugatuzi wa ufisadi na matumizi mabaya ya fedha, ilhali kaunti nyinyi zimekuwa na visa vingi vya ufisadi bila kutoa huduma, wakenya wengi wananyimwa huduma kwa sababu haya," rais Ruto aliongezea.

Rais Ruto amesema lengo sasa ni kuhakikisha kaunti zote zinatumia rasilimali zao kwa njia amabyao itaboreshwa na kujenga uchumi wao zaidi.

TRT Afrika