Mradi huo utaimarisha mfumo wa nchi wa ulinzi na kuhakikisha kwamba anga inalindwa dhidi ya tishio lolote. / Picha: AA

Uturuki imezindua mfumo wa ulinzi wa anga ambao unadhamiria kuongeza nguvu katika uwezo wake wa kulinda anga ya taifa.

Mradi huo unaoitwa 'Steel Dome' utashirikisha mfumo wa ulinzi wa anga uliopo sasa na mtandao wa kisasa zaidi, amesema Haluk Gorgun, Katibu wa katika Sekta ya Ulinzi ya Uturuki.

Mradi huo ulioasisiwa nyumbani utahakikisha kwamba mfumo wa anga wa Uturuki, pamoja na silaha zimeunganishwa. Hii itahakikisha Uturuki uwezo wa kukabiliana na tishio kwenye anga yake, kwa kasi na ufanisi wa hali ya juu, maafisa wa nchi hiyo wamesema.

Hii inatokana na uwezo mkubwa unaosaidiwa na akili mnemba, mradi huo utakuwa na vituo vya utendaji na uwezo wa kutoa maamuzi katika mazingira halisi.

'Steel Dome' ni jitihada shirikishi zinazohusisha mashirika ya Uturuki yanayoongoza katika ulinzi.

Jitihada za pamoja

Mashirika makubwa ya ulinzi ASELSAN, ROKETSAN, TUBITAK,na Ushirika wa Sekta ya Mitambo na Kemikali vyote vimejipanga kutekeleza jukumu muhimu katika kukuza mfumo huu muhimu.

Kila shirika litachangia ujuzi wake na uwezo wake wa teknolojia kuhakikisha ufanisi wa 'Steel Dome.'

Gorgun ameonesha matumaini yake kwamba mradi wa 'Steel Dome' utakuwa na manufaa makubwa kwa Uturuki, kwa maendeleo ya usalama wa taifa na ubora wa teknolojia.

Ameonesha umuhimu wa mradi huu kwa kuongeza nguvu katika miundombinu ya ulinzi na kuhakikisha kwamba anga inaendelea kulindwa dhidi ya vitisho.

TRT World