Ndege hiyo, ambayo mradi wake umeanza mwaka 2016, imezinduliwa mwezi Machi, 2023. / Picha: AA

KAAN, ni ndege ya vita iliyotengezwa Uturuki, imefanya safari yake kwanza ya majaribio, kwa mujibu wa Viwanda vya Masuala ya Anga vya Uturuki Jumatano.

Ndege ya kwanza ya kivita ya kizazi cha tano iliyotengenezwa ndani ya nchi ina lengo la kuliongezea nguvu jeshi la Uturuki.

Maendeleo ya hivi karibuni yanaifanya Uturuki kuwa moja ya nchi chache zenye teknolojia yake.

Ndege hiyo, ambayo mradi wake umeanza mwaka 2016, imezinduliwa mwezi Machi, 2023.

Ndege yenye urefu wa mita 21 inaweza kufikia kasi ya Mach 1.8 kutokana na ingini zake pacha, ambayo kila moja inaweza kuzalisha msukumo wa kilo 13, 000.

KAAN ina sifa mbalimbali kama vile uwezo wa kutambua mazingira iliyopo, kurahisisha kazi ya marubani, kuweza kutambua uharibifu uliotokea, mfumo wa kizazi kipya, uwezo wa kuona umbali wa chini, uwezo wa kulenga shabaha, na sehemu ya ndani ya kuhifadhi silaha.

Uturuki inakuza sekta yake ya ulinzi

Uturuki imekuwa yenye kuuza nje bidhaa za ulinzi, hii imechangiwa na mabadiliko chanya yaliyotokea kwa sababu serikali ya Uturuki imeamua kutengeza silaha zake yenyewe mwanzoni mwa 2000.

Tangu wakati huo, kampuni za Uturuki zimekuwa zikizalisha zana mbalimbali za ulinzi kama bunduki, magari ya vita, mifumo ya makombora, na ndege za kivita zisizo na rubani, ambazo hivi sasa zinafahamika duniani kote.

Sekta ya ulinzi ya Uturuki imechangia kwa kiwango kikubwa katika uchumi wa taifa na kufikia rekodi ya usafirishaji nje bilioni $5.5, ongezeko la asilimia 27 kutoka mwaka uliopita. Kiwango cha thamani cha wastani cha uzalishaji nje kimepita $65 kwa kilo. Ukuaji huu unaashiria kuongezeka kwa imani kwa bidhaa za ulinzi kutoka Uturuki, huku idadi ya nchi ikipokea ongezeko kutoka 176 mpaka 185.

TRT World