Tetemeko la ardhi ni mbaya zaidi katika zaidi ya karne moja. Picha: Reuters

Morocco imetangaza kukubali msaada kutoka Uhispania, Uingereza, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu kufuatia tetemeko la ardhi la kipimo cha 7 mwishoni mwa Ijumaa.

Katika taarifa iliyoandikwa Jumapili, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Morocco ilisema kuwa nchi hiyo imekubali ofa kutoka kwa mataifa hayo manne kutuma timu za utafutaji na uokoaji.

Mamlaka ilitathmini kwa uangalifu mahitaji muhimu, kwa kuzingatia matokeo yanayoweza tokea ya mapungufu ya uratibu katika hali kama hizo kufuatia tetemeko la ardhi, taarifa hiyo iliongeza.

Taarifa hiyo ilisema timu za utafutaji na uokoaji ziliingia nchini siku ya Jumapili kufanya kazi kwa uratibu na timu za Morocco, na ikasisitizwa kuwa msaada kutoka kwa nchi zingine rafiki unaweza kukubaliwa kulingana na hali ilivyo.

Pia ilieleza shukurani za Morocco kwa juhudi zinazofanywa na nchi mbalimbali.

Takriban watu 2,122 waliuawa na wengine 2,421 walijeruhiwa wakati tetemeko la ardhi la kipimo cha 7 lilipopiga Morocco mwishoni mwa Ijumaa, kulingana na Wizara ya Mambo ya Ndani.

Tetemeko hilo lilikuwa kubwa zaidi kuwahi kuikumba nchi hiyo ya Afrika Kaskazini katika karne iliyopita, kulingana na Taasisi ya Kitaifa ya Jiofizikia ya Morocco.

TRT Afrika