Mkurugenzi Mtendaji wa RwandAir ndiye mwanamke wakwanza kuwa mwenyekiti wa IATA

Mkurugenzi Mtendaji wa RwandAir ndiye mwanamke wakwanza kuwa mwenyekiti wa IATA

Mwenyekiti wa zamani Mehmet Nane akikabidhi majukumu kwa Yvonne Manzi Makolo
Makolo, ambaye amekuwa mjumbe wa bodi hiyo tangu Novemba 2020, alikua mwenyekiti wa 81 wa IATA, Picha- Rwandaa Air Twiter

Afisa mkuu mtendaji wa shirika la ndege la Rwanda RwandAir (CEO) amekuwa mwanamke wa kwanza mwenyekiti wa bodi ya magavana wa Chama cha Kimataifa cha Usafiri wa Anga (IATA).

Mwenyekiti wa zamani, Mehmet Tevfik Nane, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ndege la Uturuki Pegasus, alikabidhi majukumu kwa Yvonne Manzi Makolo siku ya Jumatatu, wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho mjini Istanbul.

Makolo, ambaye amekuwa mjumbe wa bodi hiyo tangu Novemba 2020, alikua mwenyekiti wa 81 wa IATA.

Nane ataendelea kuwa mjumbe wa bodi hiyo kwa mwaka mmoja.

AA