Upinzani nchini Kenya, ukiongozwa na Raila Odinga, uliandaa maandamano dhidi ya serikali ili kuitaka serikali kupunguza gharama za maisha na kuishawishi tume ya uchaguzi kufangua seva za kompyuta za uchaguzi mkuu wa 2022 kwa umma.
Upinzani umetilia shaka uhalali wa uchaguzi huo, licha ya mahakama ya juu kuunga mkono ushindi wa Rais William Ruto.
Pande hizo mbili,upanzani na serikali zimewasiliana na kufanya mazungumzo ya uchunguzi asubuhi ya leo kwa lengo la kushughulikia maswala muhimu, haswa ya upande wa Azimio la Umoja, ambao ulitishia kuvuruga mchakato huo.
Huu ni ushahidi wa wazi zaidi kwamba mazungumzo haya yanayopigiwa debe yanaweza kufanyika.
“Sisi wanachama wa Kenya Kwanza tumejitolea kwa utaratibu, sisi viongozi lengo letu ni utulivu na amani itawale taifa la kenya, na tutavuka kile kinachotakiwa ili hilo lifanyike’’Kimani Ichung’wah kiongozi wa wengi Bungeni kenya, alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Kikao cha kwanza kitafanyika leo katika hoteli ya Panafric jijini Nairobi kulingana na makubaliano ya dakika za mwisho yaliyoafikiwa na timu zinazomuunga mkono Rais William Ruto na kiongozi wa Upinzani Raila Odinga hapo jana.
Hatua hiyo ilichukuliwa siku moja tu baada ya uongozi wa muungano wa Azimio la Umoja kutishia kuacha mazungumzo hayo iwapo wito na uanachama wao hautapanuliwa.
Timu ya tume ya kitaifa ya uchaguzi (IEBC) inapaswa kuchaguliwa vema, seva za IEBC zifunguliwe na kukaguliwa, gharama ya maisha ijadiliwe, na makamishna wa uchaguzi waliofurushwa wakati wa uchaguzi mkuu uliopita warejeshwe kazini, kulingana na Azimio.
Hata hivyo, uongozi huo kwanza utakutana ili kusuluhisha mizozo kuhusu muundo wa kamati hiyo, haswa pingamizi la Upinzani la kujumuishwa kwa Adan Keynan, mwanachama wa Jubilee Party anayehusishwa na Azimio, kuwa mwakilishi wa muungano unaotawala.
Viongozi wa Azimio wamesema kuwa matumizi ya utaratibu za bunge katika mazungumzo hayo ulikuwa mgumu na ulihitaji kuwepo kwa wataalamu Zaidi kutoka nje ya bunge.
''Kufuatia mkutano huu, washiriki wote 14 watakutana ili kufahamu mfumo wa mazungumzo pamoja na kujadili jinsi ya kuendesha mazungumzo," alisema Bw. Otiende Amollo, mbunge wa eneo bunge la Rarieda na kiongozi wa Timu ya mazungumzo ya muungano wa Azimio la Unmoja One Kenya Coalition Party.
Licha ya makubaliano ya majadiliano na chama tawala, upinzani nchini Kenya hivi karibuni ulitangaza kuanza upya kwa maandamano ya kuipinga serikali mara baada ya mwezi wa Ramadhani.