Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Mfumo wa  IRMC imeorodhesha wote walioshtakiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ya Rwanda (ICTR) kwa uhalifu wa Mauaji ya Kimbari  nchini Rwanda mwaka 1994/ Picha ICTR

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Umoja wa Mataifa ya Rufaa ( IRMC) leo imetangaza kwamba watoro wote walioshtakiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ya Rwanda (ICTR) kwa uhalifu uliofanywa wakati wa Mauaji ya Kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda mwaka 1994, wamethibitishwa.

IRMC ilianzishwa na azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwaka 2010 ili kukamilisha kazi iliyobaki ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Rwanda na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya Yugoslavia ya zamani baada ya kukamilika kwa majukumu yao. Ina matawi mawili, moja Arusha, Tanzania, na moja The Hague, Uholanzi.

Mfumo huo umedhihirisha kuwa watoro wawili wa mwisho - Ryandikayo na Charles Sikubwabo - wamefariki.

Ryandikayo alishtakiwa kwa mara ya kwanza na ICTR mnamo Novemba 1995, pamoja na wengine wengi.

Mauaji ya kimbari ya Rwanda yalifanyika Aprili 1994 na kuwauwa zaidi ya watu laki nane / Picha AP

Mashtaka yake yalikuwa saba ambayo ni pamoja na mauaji ya halaiki, kushiriki katika mauaji ya halaiki, njama ya kufanya mauaji ya halaiki, mauaji kama uhalifu dhidi ya ubinadamu, kuangamiza kama uhalifu dhidi ya ubinadamu, ubakaji kama uhalifu dhidi ya ubinadamu na mateso kama uhalifu dhidi ya binadamu.

Sikubwabo alishtakiwa kwa mara ya kwanza na ICTR mnamo Novemba 1995. Alishtakiwa kwa mauaji ya halaiki, kushiriki katika mauaji ya halaiki, njama ya kufanya mauaji ya halaiki, mauaji kama uhalifu dhidi ya binadamu, kuangamiza kama uhalifu dhidi ya binadamu na vitendo vingine vya kinyama kama uhalifu dhidi ya binadamu.

Mnamo Julai 1994, Sikubwabo na familia yake walikimbia Rwanda na kuelekea Zaire wakati huo, ambayo sasa ni Jamhuri ya Kidemokrais ya Congo, DRC.

"Sikubwabo alitenganishwa na mkewe na watoto wadogo, ambao hatimaye walirejea Rwanda, huku Sikubwabo akisafiri hadi Jamhuri ya Congo na Jamhuri ya Afrika ya Kati kabla ya kuwasili Chad mwishoni mwa 1997," Ofisi hiyo imesema katika taarifa.

"Kufuatia uchunguzi wa kina, iligundulika kwamba Sikubwabo aliaga dunia huko N’djamena, Chad, mwaka wa 1998 na baadaye akazikwa huko," taarifa imeongezea.

Mnamo Julai 1994, Ryandikayo anaripotiwa alitoroka Rwanda na kwenda DRC. Mnamo Novemba 1996, alikuwa akiishi katika kambi ya Kashusha huko lakini, kutokana na shughuli za mapigano katika eneo hilo, Ryandikayo alikimbia kuelekea magharibi, kama walivyofanya wanaume wengine wengi wa kabila la Wahutu Wanyarwanda.

"Ryandikayo alikuwa tayari anasumbuliwa na matatizo ya kiafya kabla ya kuondoka kwake kutoka Rwanda Julai 1994, ambayo yaliongezeka wakati wa safari yake ngumu," taarifa ya mfumo wa ICTR umesema.

"Kufuatia uchunguzi wenye changamoto, Ofisi ya mwendesha mashtaka iliweza kudhihirisha kuwa Ryandikayo aliaga dunia mwaka wa 1998, uwezekano mkubwa kutokana na ugonjwa, wakati fulani baada ya kuwasili Kinshasa," imesema.

Tangu 2020, timu ya ufuatiliaji watoro ya mfumo huo wa UN umetoa hesabu ya watoro wote nane.

"Hata tunapoashiria kumaliza msako wa watoro wa mwisho wa IRMC, ni muhimu kujikumbusha kwamba bado kuna zaidi ya watoro 1,000 wanaohusihwa na mauaji ya kimbari Rwanda ambao wanatafutwa na mamlaka za kitaifa. Kuwapata itakuwa changamoto," Serge Brammertz mwendesha mashtaka wa Brammertz ameongezea.

Wawili walikamatwa ambao ni Félicien Kabuga mjini Paris, Ufaransa Mei 2020, na Fulgence Kayishema huko Paarl, Afrika Kusini Mei 2023.

Oktoba 2023, Mahakama ya Umoja wa Mataifa ya Rufaa iliamua kuwa Felicien Kabuga ni mzee na ana tatizo la akili hivyo kesi haiwezi kusikizwa.

Vifo vya watoro wengine sita vilivyothibitishwa ni vya Augustin Bizimana, Protais Mpiranya, Phénéas Munyarugarama Ndimbati, Aloys , Ryandikayo na Charles Sikubwabo.

TRT Afrika