Uturuki ina balozi 44 barani Afrika, na kuiweka kati ya nchi nne za juu za ulimwengu zenye idadi kubwa ya balozi katika bara hilo. Picha: AA

Na Brian Okoth

Hakuna rais wa nchi nyingine yeyote nje ya Afrika aliyeonesha kujali maslahi ya bara hilo kama alivyojali rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, uswahiba uliojitokeza kwa namna viongozi wa Afrika kwa jumla walivyopokea ushindi wake wa urais katika marudio ya uchaguzi.

Kutoka Nigeria hadi Somalia; Algeria hadi Afrika Kusini, harakati za Erdogan katika maendeleo, ukuaji wa uchumi na uthabiti wa kisiasa zinaweza kuonekana kwa upana.

Adamu Usman kutoka jimbo la Gombe Kaskazini Mashariki mwa Nigeria alipokea habari za ushindi wa Erdogan kwa bashasha katika mtandao wa kijamii akimtaja kiongozi huyo wa Uturuki kama ‘bingwa wa Afrika.’

Mohamed Abdi wa Somalia alimpongeza Erdogan kwa ushindi wake akisema, rais huyo ‘ameinua Uturuki na kuipa ufanisi mkubwa.’

Abdi amesema kuwa, kama raia wa Somalia amejionea binafsi ‘udugu wa kulikuwa na mamilioni ya jumbe mtandaoni – kutoka kwa marais wa mataifa mbali mbali na wanachi – wakimpomgeza Erdogan kwa ushindi wa wazi, kila mmoja akionesha taswira ya namna uongozi wa Erdogan ulivyomgusa.

Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat aliandika katika mtandao wa Twitter kuwa. ‘ Ushindi wa Erdogan unatoa fursa ya Uturuki na umoja huo kuendeleza ushirikiano wao kwa manufaa ya watu wake ".

Nguvu Mpya

Kwanini basi ushindi wa Erdogan ni muhimu kwa mataifa ya Afrika? Gitile Naituli, profesa wa usimamizi na uongozi katika chuo kikuu cha Multimedia nchini Kenya, alitaja kuendelea kwa Erdogan akatika uongozi wa taifa lake kuwa ‘Nzuri sana kwa Afrika.’

"Ushindi wake unapatia Uturuki fursa ya kupanua uwepo wake Afrika. Bara hili limefaidika kwa miaka mingi kutoka kwa Uturuki na hilo limefanikishwa na Erdogan.’’ Aliongeza

Rais Erdogan akiwa na Rais wa DRC Felix Tshisekedi (kushoto) na mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat katika Mkutano wa Ushirikiano wa Uturuki na Afrika mjini Istanbul mwaka 2021. Picha: AA

Mwanazuoni huyo amesema kuwa kiongozi mpya angechukua muda mrefu kulielewa bara Afrika na mahitaji ya watu wake, ya karibu na ya muda mrefu.

"Nchini Kenya, kwa mfano, wafanya biashara wengi wa nguo wanaingiza bidhaa zao kutoka Uturuki. Ndege ya kitaifa ya Uturuki, inasafiri maeneo mengi barani Afrika, pengine mara nyingi zaidi kuliko ndege nyingine yoyote ya kigeni, na tunaona wasafiri wengi zaidi kwenda na kurudi kutoka Uturuki. Ushindi wa Erdogan una maana kuwa kiwango hiki cha biashara kitakithiri,’’ Naituli aelezea.

Macharia Munene, mhadhiri wa mahusiano ya kimataifa katika chuo kikuu cha USIU Afrika, amesema kuwa, ‘’ushindi wa Erdogan unampa ‘nguvu zaidi kuendeleza miradi aliyoanzisha barani Afrika.’’

“Ushindi huu sio tu kumpa fursa kuikuza Uturuki zaidi, bali pia unamuwezesha kupanua zaidi ushirikiano na Afrika katika masuala kama ya diplomasia na biashara,’’ amesema Munene.

Uwepo wa Uturuki barani Afrika unagusia Nyanja mbali mbali ikiwemo, uchumi, diplomasia, kibinadamu, elimu na afya. Wakati Erdogan, alipokuwa waziri mkuu 2003-2014, aliweka mambo sawa kuwezesha ushirikiano na uhusiano mwema na mataifa ya Afrika.

Na ili kuthibitisha uhusiano huu, alifanya ziara nyingi barani Afrika. Chad, Somalia, Sudan, Tunisia, Senegal, Ethiopia, Angola, Nigeria na Togo ni miongoni mwa zaidi ya mataifa 30 alizopitia kufikia sasa, ikiwa idadi kubwa zaidi ikilinganishwa na rais mwingine yeyote wa sasa au wa zamani.

Uwezo wa Afrika

Naituli amesema kuwa rais Erdogan amekuwa "mjanja zaidi kuelewa uwezo wa kibiashara wa Afrika".

"Bara hili lina zaidi ya watu Bilioni 1.4, na ni soko linalokua ambalo bado halijatambulika. Erdogan ameona nafasi hiyo na ameamua kufanyia kazi hilo," amesema.

Rais huyo kwa mfano anafahamu kuwa, ili ushirikiano wa kiuchumi ufanikishwe, lazima kwanza kuwekeza katika elimu.

"Hii inaeleza kwanini alizindua miradi mingi ya elimu barani Afrika na kutoa msaada wa elimu kwa wanafunzi wengi barani. Elimu ndio mwanzo wa biashara kwasababu mtu aliye na ufahamu zaidi anakuwa mbunifu, anaelewa na kujinasibisha na maendeleo," anasema Naituli.

Zaidi ya wanafunzi 14,000 walio na talanta wamenufaika na msaada wa elimu kutoka Uturuki huku wanadiplomasia zaidi ya 250 wakipewa mafunzo maalum.

Uturuki inatumia shirika la kimataifa la elimu, wakfu wa Maarif, na baraza la lugha ya kituruki, taasisi ya Emre Yunus, kukuza hili. Munene anasema kuwa Erdogan amefanikiwa kuweka wazi ‘’maono ya Uturuki kwa Afrika ".

Ushirikiano wa ki mkakati

Kwa mujibu wa Dkt Edgar Githua, mtaalamu wa masuala ya uhusiano wa kimataifa, Jukumu la Uturuki barani Afrika linagusia pia mikakati ya kiusalama.

"Afrika ni mshirika muhimu wa rais Erdogan, nan chi hiyo ni gwiji wa masuala ya kuweka amani na diplomasia ya kimataifa,’’ anasema. Githua pia anaamini Uturuki ni mshirika muhimu sana katika kuhakikisha usalama wa chakula barani Afrika.

"Makubaliano ya nafaka ya bahari nyeusi ni ushuhuda wa jukumu la Uturuki katika kuhakikisha usalama wa chakula barani. Rais Erdogan alipo ongeza mkataba wa nafaka kwa miezi miwili mnamo mwezi Meim alisema kuwa alifanya kwa maslahi ya waafrika.

Urusi na Ukrain ndio wanaongoza kwa uzalishaji wa nafaka duniani n auturuki husaidia katika kuwezesha upitishaji wa nafaka hiyo hadi Afrika kupitia bahari nyeusi.

Sera ya kuto-kuingilia

Githua anasema kuwa Uturuki inapata mapokezi mazuri barani Afrika kwasababu, ‘’ tofauti na nchi nyingi za magharibi, haiingilii siasa za ndani za mataifa hayo."

"Uturuki haitakuambia nani wa kumchagua kama rais au namna ya kuishi. Wao wanataka tu kufanya biashara na wewe na kuhakikisha unafaidika,’’ aliambia TRT Afrika.

Mtaalamu huyo wa mahusiano ya kimataifa anabashiri kuwa huenda Erdogan akaangazia zaidi njia za kupanua uhusiano wake na Afrika katika masuala ya kiuchumi, kidiplomasia, na ulinzi katika kipindi chamiaka mitano ijayo.

"Huenda pia akabeba jukumu muhimu la kuweka uslama barani Afrika,’’ anasema Githua.

Takwimu zinaonesha wazi upana wa uhusiano endelevu kati ya Uturuki na bara Afrika.

Kuna mabalozi 44 za uturuki barani, hivyo kuiweka nchi hiyo miongoni mwa mataifa manne ya juu zaidi duniani yaliyo na mabalozi wengi zaidi barani, nyum aya China (53), Marekani (49) na Ufaransa (46).

Katika sekta ya afya, ni vigumu kukosa kuona uwepo wa Uturuki Afrika. Mfano, katika mjimkuu wa Somalia, Mogadishu, Erdogan alijenga hospitali kubwa zaidi 2015, lililopewa jina lake.

Nchini Senegal, Uturuki imezindua miradi kadhaa, ikiwemo uwanja wa kimataifa wa Abdoulaye Wade, wenye uwezo wa kubeba watu 50,000 uliojengwa na kampuni ya Summa katika kipindi cha miezi 17 tu,kuanzia Februari 2020.

Rais Erdogan amezuru Senegal mara nne. Nchini Tanzania, kampuni ya Uturuki ya Yapi Merkezi ilipewa kandarasi kutengeneza reli ya SGR. Ubora wa kazi yake ulipata sifa kutoka kwa serikali ya Uganda.

"Yapi Merkezi inasemekana kufanya kazi ya hali ya juu katik aujenzi wa SGR nchini Tanzania," serikali ya Uganda ilisema katik amtandao wa Twitter Mei 16, ilipotangaza kurejea ujenzi katika reli ya SGR kutoka Kampala – Kigali.

Nchini Rwanda, kampuni ya Uturuki ndio iliyojenga ukumbi wa Kigali wa BK, utakaotumika kwa shughuli mbali mbali na uwezo wa kupokea watu 10,000. Uturuki pia imehusika katika shughuli za misaada katika nchi mbali mbali ikiwakilishwana Tika, shirika la uturuki la ushirikiano na uratibu.

Faida kwa pande zote

Kawi, ulinzi, mavazi, filamu, usafiri na vifaa vya kijeshi, nimambo ambayo Uturuki imeweza kufaidi nayo mataifa mengi ya Afrika.

"Kupitia sera yetu ya ushirikiano wa Afrika, ambao unatokana na uelewa wa pamoja unaohusisha shughuli za taasisi za umma, sekta ya kibinafsi, mashirika yasio ya kiserikali na mashirika ya misaada, tunalenga kuchangia katika usalama, uthabiti, uchumi na maendeleo ya kijamii barani Afrika, na kuendeleza mahusiano yatu kwa manufaa ya pande zote.’’ Amesema waziri wa mambo ya nje wa Uturuki.

AKiongoza taifa kwa miaka mitano nyingine Afrika ina uhakika kuwa uongozi wa Erdogan utaendelea kuleta mambo mazuri. Pande zote mbili zina Imani na mwenzake.

"kunao wale ambao bado hawakubali uhuru wa nchi, na mafanikio ya usawa ya watu wa Afrika. Kama Uturuki, tunapinga mitazamo ya ubinafsi ya nchi za magharibi juu ya masuala ya Afrika. Tunawakubali watu wa Afrika bila ubaguzi," rais alisema Oktoba 2021.

Biashara na wengi

Mnamo 2022, Mauzo ya Uturuki kwa Afrika ilipita $21 bilioni na kufikia viwango vya kihistoria. Mauzo hayo yaliongezeka kwa 12.3% ikilimganishwa na 2021.

Misri ($3.9 bilioni), Morocco ($3 bilioni), Libya ($2.4 bilioni), Algeria ($1.9 bilioni) na Afrika Kusini ($1.6 bilioni) ndiyo mataifa ya Afrika ambayo Uturuki iliuzia bidhaa zaidi.

Kemikali, nafaka, mafuta na bidhaa za viwanda, mafuta ya zaituni, matunda mboga na magari pamoja na vifaa vya ujenzi ndivyo vitu vilivyouzwa kwa wingi Afrika kutoka Uturuki.

Uturuki inaagiza mafuta ghafi, dhahabu, chuma, gesi asili ya maji, na mali nyingine ghafi kutoka Afrika.

Kwa mujibu wa data rasmi kutoka halmashauri ya takwimu ya Uturuki, juml aya mauzo kutoka Afrika kwa Uturuki, ilifikia $8.3 bilioni 2021, huku mafuta ghafi ikiongoza katika mauzo hayo.

"Kwa ushindi wa Erdogan tunatarajia biashara zaidi ya pande mbili kati ya Afrika na Uturuki kwasababu hakutakuwana muingi;lio wa kisiasa. Ushindi wake unatuhakikishia upanuzi endelevu kwa sekta mpya za biashara," anasema Naituli.

Githua anabashiri kutokea mikutano zaidi ya ushirikiano kati ya Uturuki na Afrika katika muhula mpya wa Erdogan.

"Atataka kuimarisha zaidi uwepo wa Uturuki barani Afrika. Ushindi katika uchaguzi wa urais unampa Erdogan uhalali na nguvu zaidi kuunganisha Uturuki, kuzidisha mara mbili ushirikiano na Afrika na kufikia Nyanja ambazo bado hazzijaguswa barani.."

Erdogan alishinda marudio ya uchaguzi ya Mei 28 baada ya kunyakua 52.18% ya kura dhidi ya mpinzani wake Kemal Kilicdaroglu aliyapata 47.82% ya kura.

Uchaguzi huo ulipelekwa kwa marudio baada ya wagombea wote kukosa kushindwa kupata asili mia 50 na kura moja katika uchaguzi uliofanyika Mei 14, japo bado Erdogan alikuwa anaongoza.

TRT Afrika