Kiongozi wa upinzani wa Urusi aliyekuwa amefungwa, Alexey Navalny amefariki, hayo ni kwa mujibu wa kitengo cha magereza kutoka jimbo la Yamalo-Nenets ambapo amekuwa akitumikia kifungo.
Katika taarifa iliyochapishwa mtandaoni wake siku ya Ijumaa, Huduma ya Shirikisho ya Magereza katika wilaya ya Yamalo-Nenets imesema kuwa Navalny "alijihisi kuumwa" baada ya kutoka kutembea siku ya Ijumaa, na "muda mfupi baadae kupoteza fahamu."
Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa, watumishi wa afya wameitwa, lakini wameshindwa kumsaidia Navalny kupumua tena. Imesema chanzo cha kifo chake kinachunguzwa.
TRT World