Rais Samia akisikiliza maelezo kutoka kwa wananchi. Picha/Ikulu

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa eneo la Jorodom ambalo limeathirika na Mafuriko pamoja na maporomoko ya matope na mawe Wilayani Hanang Mkoani Manyara. Rais Samia alijionea uharibifu mkubwa uliotokea na kuwapa pole waathirika wa maafa hayo na kuwaeleza kuwa Serikali ipo pamoja nao.

Eneo la Jorodom, lililopo Katesh ni miongoni mwa maeneo yaliyoathirika zaidi. Picha/Ikulu

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Elibariki Naman, ambae ni mkazi wa Jorodom, Katesh mmoja wa waathirika wa mafuriko yaliyotokea Wilayani Hanang. Elibariki alikuwa akielezea jinsi majirani zake walivyopoteza maisha pamoja na makazi yao katika maafa hayo.

Rais Samia akipata maelezo kutoka kwa uongozi wa Mkoa wa Manyara. Picha/Ikulu

Rais Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga akielezea athari za mafuriko yaliyotokea katika eneo la Jorodom Katesh Wilayani Hanang.

Rais Samia aliwatembelea majeruhi wa maafa ya mafuriko hayo ambao wamelazwa katika hospitali ya Wilaya Mkoani Manyara.

Rais Samia Suluhu Hassan akimfariji muathirika wa mafuriko yaliyotokea Katesh Bi. Salome Elifuraha ambaye amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tumaini iliyopo Katesh, Hanang. Mama amepoteza watoto wawili kwenye maafa hayo huku mtoto wa tatu akiwa bado hajapatikana hadi sasa.

TRT Afrika