Israel inajaribu kuzima sauti yoyote yenye ukweli kutoka Gaza kwa kuwashambulia bila aibu waandishi wa habari ambao wanafanya kazi yao. Picha/AA.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Uturuki amelaani vikali "Israel inavyoshambulia waandishi kwa kudhamiria" na "kampeni ya Israel ya kuinyima dunia haki ya kupata picha halisi ya kinachoendelea."

"Tumeshangazwa sana na kuuawa kwa mwenzetu mwengine, Mohammad Abu Hattab, mwandishi wa Palestine, pamoja na wana familia yake 11 kutokana na shambulizi la anga la Israel. Nataka kutoa salam zangu za rambirambi kwa wana familia, ambao wameuawa katika shambulio hili la kioga," Fahrettin Altun amesema kupitia mtandao wa X.

"Huu ugaidi sharti usitishwe. Ulimwengu uliostaarabika lazima utilie maanani kwa kuzuia huu uwanda wazimu," ameongeza Mkurungenzi huyo wa Mawasiliano.

Akikumbusha kwamba waandishi 38 tayari wameuawa kutokana na mashambulizi ya Israel Gaza tangu Oktoba 7, Altun amesema kuendelea kukiukwa kwa haki za binadamu katika eneo la Gaza iliyozingirwa "hakukubaliki."

Amegusia kwamba, idadi kubwa ya vifo ni ya watoto, wanawake na wazee, wahudumu wa afya, na waandishi wa habari, Altun amesema mashambulizi yanayolenga wote ya Israel dhidi ya wananchi yameonyesha picha mbaya ya vifo vya maelfu ya raia.

"Kudhalilishwa kwa wananchi wa Gaza kumefikia kiwango cha juu kabisa. Israel pia inajaribu kuziba sauti za kweli kutoka Gaza bila aibu kwa kushambulia waandishi wa habari ambao wanafanya kazi yao."

Waandishi wanakabiliwa na hatari kubwa

Akiwakumbusha uhuru wa vyombo vya habari na haki ya dunia kupata taarifa sahihi, Altun amesema, Israel "ni wazi inataka upande wao wa habari kuonekana kupitia vyombo vya habari."

"Jumuia ya kimataifa imeshindwa kuwashurutisha Israel kuhusu mashambulizi yake kwa vyombo vya habari, lazima sharti ifanye hivyo hata kama imechelewa kwa wenzetu wengi," ameongeza kusema.

Jeshi la Israel limeongeza mashambulizi yake ya anga Gaza, ambayo imekuwa ikishambuliwa kupitia anga tangu kufanyika kwa shambulizi la Hamas Oktoba 7.

Takriban watu 10,600 wameuawa katika mgogoro huo, ikiwemo Wapalestina 9,061 na zaidi ya Waisrael 1,538.

Mbali na idadi hiyo kubwa ya vifo na watu kukosa makazi, huduma muhimu zinaendelea kukosekana kwa wakazi wa Gaza 2.3 kutokana na zuio la Israel.

Waandishi wa habari Gaza wanakabiliwa na tishio kubwa huku wakijaribu kutoa habari za mgogoro huo kwa kuonyesha uvamizi wa Israel, mashambulio ya anga ya Israel yanayotisha, kusitishwa kwa mawasiliano, na kukatwa kwa huduma ya umeme, kwa mujibu wa Kamati ya Kulinda Waandishi.

TRT Afrika