Na Coletta Wanjohi
TRT Afrika, Antalya Uturuki
Viongozi wa ngazi mbali mbali wanakutana mjini Antalya nchini Uturuki kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Diplomasia wa Antalya yani Antalya Diplomacy Forum.
Mkutano huu unafanyika kuanzia tarehe moja hadi 3 Machi, chini ya usimamizi wa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
Hii ni awamu ya tatu ya mkutano huu wa kila mwaka ambayo inawaleta pamoja, marais wa nchi tofauti, wakuu wa serikali, mawaziri, wanadiplomasia, viongozi wa biashara, wasomi, na wataalamu.
Mada kuu ya Jukwaa la mwaka huu itakuwa ni, “Kuendeleza Diplomasia katika Nyakati za Machafuko."
Afrika imewakilishwa na viongozi wa ngazi mbali mbali kutoka nchi kama Eswatini, Afrika Kusini, Zimbabwe, Tanzania, Mali, Burkina Faso na Somalia.
Mkutano wa Diplomasia wa Antalya unalenga kutumika kama tafakari ya kina na njia za kutafuta njia ya amani kutoka kipindi cha msukosuko ambacho ulimwengu unapitia.