AFCON: Wanigeria wanaoishi Afrika Kusini waonywa dhidi ya kushangilia sana iwapo watashinda

AFCON: Wanigeria wanaoishi Afrika Kusini waonywa dhidi ya kushangilia sana iwapo watashinda

Tahadhari hiyo ilitolewa kupitia taarifa ya ubalozi wa Nigeria Nchini Afrika Kusini
Mashabiki wa Nigeria Afcon / Picha: Reuters

Ubalozi wa Nigeria Nchini Afrika Kusini umewahimiza Wanigeria kufuata sheria kabla, wakati na baada ya mechi ya nusu fainali ya Afcon kati ya Nigeria na Afrika Kusini.

"Ubalozi unashauri jamii ya Nigeria kuwa waangalifu juu ya matamshi yao, kuwa waangalifu juu ya wapi wanachagua kutazama mechi hiyo haswa katika maeneo ya wazi, na kujiepusha na kushiriki katika sherehe kubwa, za fujo au za kuchochea ikiwa Super Eagles watashinda mechi hiyo." Ubalozi ilisema.

Super Eagles na Bafana Bafana zitapambana katika Uwanja wa Stade de La Paix, Bouake Jumatano usiku.

TRT Afrika na mashirika ya habari