Vilio na mayoe vimetawala katika eneo la Se'me' Krakre', lililopo katika mpaka wa nchi ya Benin na Nigeria. Hii ni baada ya moto mkali kuanza katika ghala la mafuta ya petroli na kuunguza kila kitu huku ukisababisha vifo vya takriban watu 30 na uharibu mkubwa wa mali. Hayo ni kutokana na taarifa za vyombo vya habari vya ndani ya Benin.
Picha za kutisha zinazoenea katika mitandao ya kijamii zinaonyesha watu wakipiga kelele na kuomba msaada huku moshi mkubwa wenye rangi weusi ukionekana katika eneo la tukio.
Majanga ya moto unaosababishwa na vitendo haramu yamekuwa yakitokea mara kwa mara katika maeneo mbalimbali barani Afrika na kusababisha madhara makubwa ikiwemo vifa na uharibifu wa mali. Hata hivyo, ni hatua chache zinazoonekana kuchukuliwa hasa baada ya majanga hayo kutokea.