Maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi yanayoitwa 'Me Emme Vaikene!' (Hatutanyamaza) imefanyika huko Helsinki siku ya Jumapili. TRT 

Maelfu ya watu walikusanyika katika mji mkuu wa Finland, Helsinki, kupinga ubaguzi wa rangi na sera ya serikali juu ya ubaguzi, kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya ndani.

Zaidi ya waandamanaji 10,000 na wanachama wa zaidi ya mashirika 100, ikiwa ni pamoja na mashirika ya haki za binadamu, walikusanyika katika uwanja wa Seneti wa Helsinki na baadaye kuelekea bustani ya Toolonlahti siku ya Jumapili, ilisema shirika la utangazaji la YLE.

Walielezea kusikitishwa kwao na sera ya serikali dhidi ya ubaguzi wa rangi, wakiongelea mkutano wao wa kupinga ubaguzi wa rangi wiki iliyopita.

Waandamanaji waliitaka serikali kuheshimu katiba ya Finland na mikataba ya kimataifa ambayo wametia saini, ilisema ripoti hiyo.

Kashfa za ubaguzi wa rangi

Siku ya Alhamisi, vyama vya serikali ya mseto nchini Finland vilifichua taarifa ya pamoja juu ya kutokomeza ubaguzi wa rangi na kukuza usawa ndani ya jamii ya Finland.

Hayo yamejiri baada ya msururu wa kashfa za ubaguzi wa rangi zilizohusisha mawaziri zilizokumba serikali mpya na kusababisha kuteuliwa kwa jopokazi lililopewa jukumu la kupendekeza hatua madhubuti za kukabiliana na ubaguzi wa rangi na ubaguzi.

Mnamo Juni, serikali ya vyama vinne, ikiwa ni pamoja na Chama cha Finns kinachopinga uhamiaji, kiliunda serikali mpya ya Finland, ambayo inashikilia viti 108 kati ya 200 bungeni.

TRT World