Zaidi ya miaka 230 tangu meli za kwanza za Uingereza kutia nanga mjini Sydney, Waziri Mkuu Anthony Albanese alipendekeza mageuzi hayo kama hatua ya kuelekea maridhiano ya watu wa rangi tofauti. : AFP

Raia wa Australia wamekataa haki kubwa zaidi kwa raia wa kiasili, wakipuuza mipango ya kurekebisha katiba ya nchi hiyo iliyodumu kwa miaka 122 baada ya kampeni ya kura ya maoni yenye mgawanyiko na yenye ubaguzi wa rangi.

Huku theluthi mbili ya maeneo ya kupigia kura yakiripoti matokeo, asilimia 55 ya wapiga kura walipiga kura ya "hapana" kuwatambua Waaboriginal na Wakazi wa Visiwa vya Torres Strait katika katiba ya nchi kwa mara ya kwanza.

Marekebisho hayo pia yangeunda chombo cha mashauriano - "Sauti" kwa Bunge - kuratibu sheria zinazoathiri jamii za wenyeji na kusaidia kushughulikia kukosekana kwa usawa wa kijamii na kiuchumi.

Licha ya kuungwa mkono na serikali ya mrengo wa kati nchini humo, kampeni ya "ndio" ilikuwa imeonesha kukosa uungwaji mkono katika kura za maoni kwa miezi kadhaa, na kushindwa kwake kulitarajiwa kwa kiasi kikubwa.

Umwagaji damu wakati wa ukoloni zamani

Naibu Waziri Mkuu Richard Marles alikiri kushindwa mapema jioni, akiambia shirika la utangazaji la ABC "Waaustralia hawajapigia kura mabadiliko ya katiba."

Licha ya kura za maoni za kabla ya kufanyika kura hii , Waaustralia wa Asili walionyesha hasira na uchungu kwamba weupe walio wengi walikataa wito wa kutambua ukoloni wa zamani wa umwagaji damu.

"Haya ni matokeo magumu, haya ni matokeo magumu sana," alisema mkurugenzi wa kampeni wa Yes23 iliyokuw aikiunga mkono kura hiyo, Dean Parkin.

"Tulifanya kila tuliloweza na tutarejea kutoka kwa hili," alisema.

Upatanisho wa watu wa rangi tofauti

Zaidi ya miaka 230 tangu meli za kwanza za Uingereza kutia nanga mjini Sydney, Waziri Mkuu Anthony Albanese alipendekeza mageuzi hayo kama hatua ya kuelekea maridhiano ya rangi.

Lakini badala yake, imezua mjadala mkali na uliojaa ubaguzi wa rangi ambao ulifichua pengo kati ya watu wa asili ya Kiaborijin na weupe walio wengi.

Kura za maoni zimeonyesha mara kwa mara kwamba wapiga kura - ambao wengi wao ni wazungu - huweka masuala ya wenyeji chini ya orodha yao ya vipaumbele vya kisiasa.

Katika siku chache kabla ya kupiga kura, umakini wa vyombo vya habari umezingatia zaidi matukio ya Mashariki ya Kati kama mjadala wa kisiasa wa nyumbani.

Kampeni ya upinzani ilielekeza kwa ustadi hofu juu ya jukumu na ufanisi wa mkutano wa "Sauti", kuwahimiza watu kupiga kura ya "hapana" ikiwa hawana uhakika.

Taarifa potofu mtandanoni

Mjadala huo uliambatana na taarifa potofu za mtandaoni: kupendekeza "Sauti" ingesababisha unyakuzi wa ardhi, mfumo wa ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini au ulikuwa sehemu ya njama za Umoja wa Mataifa.

Kiongozi wa kiasili Thomas Mayo alielezea kukerwa na mwenendo wa kampeni ya "Hapana", ambayo iliungwa mkono na kiongozi wa upinzani wa kihafidhina Peter Dutton.

"Wamedanganya watu wa Australia. Ukosefu huu wa uaminifu haufai kusahaulika katika demokrasia yetu na watu wa Australia," alisema.

"Kunapaswa kuwa na athari kwa aina hiyo ya tabia katika demokrasia yetu. Hawapaswi kuachiwa kwa hili."

Mashtaka ya ubaguzi wa rangi

Dee Duchesne, 60, mfanyakazi wa kujitolea kwa kampeni ya "hapana", alisema "anapigania kuweka safu ya ziada ya urasimu nje ya katiba yetu".

Alisema alikuwa ameitwa mbaguzi wa rangi alipokuwa akisambaza vipeperushi karibu na kituo cha kupigia kura cha Sydney wakati wa upigaji kura wa mapema. "Mimi sio mbaguzi," alisema.

Kupiga kura ni lazima kwa wapiga kura milioni 17.6 wa Australia.

Kura ya maoni inaweza tu kupita kwa kuungwa mkono na wapiga kura wengi kitaifa na wengi wa wapiga kura katika angalau majimbo manne kati ya sita ya nchi.

Ilishindwa kuwavutia wote .

Kura ya maoni ilikuwa inauliza: "Sheria Inayopendekezwa: kubadilisha Katiba ili kutambua Watu wa Kwanza wa Australia kwa kuanzisha Sauti ya Waaboriginal na Torres Strait Islander. Je, unaidhinisha mabadiliko haya yaliyopendekezwa?"

TRT World