Takriban Waisrael 1400 wameuawa katika mzozo huo. / Picha: AA

Jumatatu, Oktoba 16, 2023

1732 GMT - Hilali Nyekundu ya Uturuki inaendelea kutoa msaada kwa Wapalestina katika Gaza

Hilali Nyekundu ya Uturuki inaendelea kutoa msaada wa kibinadamu kwa Wapalestina wanaoathiriwa na mashambulizi ya Israel huko Gaza.

Hilali Nyekundu ya Uturuki ilisema kwenye taarifa yake Jumatatu kwamba inashirikiana na timu za ndani kugawa msaada wa kibinadamu kwa sababu hakuna wafanyakazi wa misaada kutoka nje wanaoweza kuingia Gaza.

Taarifa hiyo ilibainisha kuwa Hilali Nyekundu ya Uturuki inatafuta njia ya kuanzisha korido au njia salama ya kibinadamu ili kuleta vifaa vya misaada kutoka nje ya Gaza.

Nchi kadhaa zimetuma misaada na vifaa vya kibinadamu kwa watu wa Palestina huko Gaza, lakini vifaa hivi vimenaswa karibu na mipaka ya Misri kwani Israeli inaendelea kukataa kuruhusu msaada kuingia Gaza.

1623 GMT - Netanyahu ana imani na 'ushindi wa Israel dhidi ya Hamas'

Israel inalenga kuwashinda kundi la Palestina la Hamas na kumaliza utawala wake Gaza, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema Jumatatu.

Akizungumza na Knesset, bunge la Israel, kabla ya operesheni ya ardhini inayotarajiwa, Netanyahu alisema "lengo letu ni ushindi dhidi ya Hamas, kuiondoa kutoka madarakani."

"Tutashinda, kwa sababu kuwepo kwetu hapa kupo hatarini," Netanyahu alisema, kulingana na Times of Israel mtandaoni, na akaendelea kuelezea kundi la Hamas kama "Hamas ya Nazi."

Waziri Mkuu wa Israel pia aliwaonya Iran na Hezbollah dhidi ya kuingilia kati mapambano kati ya Israel na makundi ya Palestina huko Gaza.

0922 GMT — Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Sameh Shoukry amesema kuwa Cairo ina lengo la kuweka kivuko cha Rafah kufanya kazi tangu mzozo huo ulipozuka, huku kukiwa na mashambulizi ya Israel ya Gaza, huku hali ya kibinadamu ikizidi kuwa mbaya katika eneo la Palestina.

"Hadi sasa, kwa bahati mbaya, serikali ya Israel haijachukua msimamo unaoruhusu kivuko hicho kuwa wazi kutoka upande wa Gaza," Shoukry alisema.

Mwanadiplomasia huyo mkongwe wa Misri pia alisisitiza kwamba kile ambacho Wapalestina wa Gaza wanakabiliana nacho ni "hatari."

0716GMT - Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu imekanusha ripoti za kusitishwa kwa mapigano huko Gaza ambayo yatawezesha misaada kuingia na wageni kukimbilia Misri, siku 10 katika vita na Hamas.

"Kwa sasa hakuna usitishaji vita na misaada ya kibinadamu huko Gaza kwa kuwaondoa wageni," taarifa kutoka ofisi ya Netanyahu ilisema.

Kwa upande wake, afisa wa Hamas Izzat El Reshiq ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba hakuna ukweli wowote kuhusu taarifa kuhusu kufunguliwa kwa kivuko cha mpaka cha Rafah na Misri au kusitishwa kwa mapigano kwa muda.

0157 GMT - Rais wa Marekani Joe Biden anafikiria safari ya Israeli katika siku zijazo lakini hakuna thibitisho , afisa mkuu wa utawala alisema.

Safari inaweza kuwa nafasi kwa Biden kuthibitisha kibinafsi kwa watu wa Israeli ambao Amerika inasimama kidete nyuma yao. Lakini itakuja huku kukiwa na hofu kubwa kwamba hatua inayokuja ya Israel kuingia Gaza inaweza kuzua vita vikubwa na matokeo mabaya ya kibinadamu.

0148 GMT - UN: Gaza inanyongwa bila maji, chakula au dawa

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Palestina linasema Gaza "inasakamwa" na idadi ya watu wanaotafuta hifadhi katika shule na vituo vyao kusini mwa eneo hilo ni kubwa mno.

"Tukiangalia suala la maji - sote tunajua maji ni uhai - Gaza inakosa maji, na Gaza inaishiwa na maisha," Philippe Lazzarini, kamishna mkuu wa UNRWA katika mkutano na waandishi wa habari mjini Jerusalem.

"Hivi karibuni, ninaamini, na hii hakutakuwa na chakula au dawa pia," alisema.

"Shambulio la wiki iliyopita dhidi ya Israeli lilikuwa la kutisha," alisema.

"Shambulio hilo na kukamatwa kwa mateka ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa za kibinadamu. Lakini jibu la mauaji ya raia haliwezi kuwa kuua raia zaidi.”

0113 GMT - Vikosi vya Israel vinaendelea kushambulia Gaza

Jeshi la Israel liliendelea kushambulia maeneo ya Gaza kwa mashambulizi ya anga kwa siku ya tisa mfululizo huku eneo la Palestina lililozingirwa likikabiliwa na mzozo wa dharura wa kibinadamu.

Walioshuhudia tukio hilo waliliambia Shirika la Habari la Anadolu kwamba idadi kubwa ya watu waliuawa na wafanyakazi wa ulinzi wa kiraia na gari la wagonjwa walijeruhiwa walipokuwa wakielekea mtaa wa Al Jalaa huko Gaza kuwaokoa majeruhi.

0122 GMT - Hospitali za Gaza zimezidiwa na wagonjwa na zinashindw akukidhi mahitaji wakati uvamizi unakaribia

Madaktari wa Gaza walionya kuwa maelfu wanaweza kufa kwani hospitali zilizojaa watu waliojeruhiwa zinakabiliwa na upungufu wa mafuta na vifaa vya kimsingi.

0040 GMT - Waandamanaji waandamana Morocco, Iraqi kwa mshikamano na Wapalestina

Waandamanaji waliandamana nchini Morocco na Iraq kwa mshikamano na Wapalestina na kupinga mashambulizi ya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza, ambayo yamesababisha maelfu ya vifo vya raia.

Wakati wa maandamano katika mji wa Marrakesh nchini Morocco ulioitishwa na mashirika kadhaa yasiyo ya kiserikali, waandamanaji walibeba bendera na mabango ya Palestina kumulika kadhia ya Palestina.

0030 GMT - Biden anasema kukaliwa kwa Israeli huko Gaza itakuwa 'kosa kubwa'

Rais wa Marekani Joe Biden alisema kuwa kuikalia kwa Israel Gaza itakuwa "kosa kubwa" lakini inaonekana sawa kwa operesheni ya ndani dhidi ya kundi la Palestina Hamas.

"Nadhani itakuwa kosa kubwa," Biden alisema katika mahojiano na kipindi cha Dakika 60 cha CBS News.

TRT World