Takriban watoto milioni 67 wamekosa kabisa au hawajapata chanjo zote kati ya 2019 na 2021 kutokana na vizuizi katika huduma za afya vilivyo sababishwa na janga la Covid-19, UNICEF ilisema katika ripoti mpya.
Kati ya hao, milioni 48 walikosa kabisa nafasi hiyo, ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, iliyopewa jina la "Hali ya Watoto Duniani 2023: Kwa Kila Mtoto, Chanjo" ilichapisha taarifa hiyo Jumatano.
"Chanjo huokoa maisha, lakini watoto wengi sana ulimwenguni hawapati chanjo.
Janga la Uviko-19 liliongeza idadi yao," ilisema ripoti hiyo. Ilisema kwamba "katika miaka mitatu iliyopita, zaidi ya muongo mmoja wa mafanikio yaliyopatikana kwa bidii katika chanjo ya kawaida ya utotoni yamemomonyoka," na kuongeza kuwa kurejea kwenye mstari itakuwa vigumu.
"Katika asilimia, sehemu ya watoto waliopatiwa chanjo ilishuka kwa asilimia 5 hadi asilimia 81. Kwa maneno mengine, karibu mtoto mmoja kati ya watano duniani kote hawakuwa na ulinzi kamili dhidi ya magonjwa yanayoweza kuzuilika."
Kulingana na takwimu, imani katika chanjo za watoto ilipungua kwa asilimia 44 katika baadhi ya nchi wakati wa janga hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Catherine Russell alisema data hiyo ni ishara ya onyo linalotia wasiwasi.