Mtandao wa  TikTok / Photo: AP

Wabunge wa Montana walitoa kibali cha mwisho mnamo Ijumaa kwa mswada wa kupiga marufuku programu ya media ya kijamii ya TikTok kufanya kazi katika jimbo hilo, hatua ambayo itakabiliwa na changamoto za kisheria

Mchakato huu unakuja siku chache baada ya mkurugenzi wa Tiktok kuhojiwa nchini Marekani.

Hivyo maamuzi dhidi ya programu hiyo maarufu sasa yanangoja kutiwa saini na gavana wa Republican lakini inatarajiwa kuwepo na changamoto za kisheria

Baraza la serikali lilipiga kura 54-43 kupitisha muswada huo, iko marufuku iliyowekwa katika karibu nusu ya majimbo na serikali ya shirikisho la Amerika ambayo inakataza TikTok kwenye vifaa vya serikali.

Ambapo kwa upande wa jimbo la Montana tayari wamepiga marufuku programu hiyo kwenye vifaa vinavyo milikiwa na serikali.

Mtandao wa tiktok unazidi kupata umaarufu mkubwa duniani huku taifa la Marekani likipinga vikali mtandao huo kwa kushutumu kuwa unatumiwa na China kuhatarisha usalama wa taarifa za watu na hasa nchi hiyo kwa ujumla.

TRT Afrika