Mkurugenzi wa CIA William Burns, mkuu wa Mossad David Barnea, na Waziri Mkuu wa Qatar Al Thani walikutana na maafisa wa Misri Mjini Cairo "kujadili makubaliano ya kusitisha Mapigano huko Gaza", vyombo vya habari nchini Misri vimeripoti
Shirika hilo la Misri, Al Qahera liliripoti uwepo wa mkutano huo huku kukiwepo shinikizo kutoka jumuiya ya kimataifa kufanikisha mazungumzo ya amani kati ya Israel na kikundi cha Hamas , kutoka Palestina.
Shirika la kijasusi la Israel limesisitiza kuwa linatathmini majibu ya Hamas kwa mpango uliopendekezwa wa kusitisha mapigano huko gaza, ambapo zaidi ya watu 28,000 wamekwishauwawa
Mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza ambayo sasa yameingia katika siku yake ya 130 — vimeua Wapalestina wasiopungua 28,473 na kuwajeruhi wengine 68,146, huku mashambulizi ya anga ya Israel yakiendelea kuupiga mji wa Rafah.