Rais wa Urusi Vladimir Putin na viongozi wa Afrika katika mkutano wa Urusi na Afrika  / Photo: Reuters

Urusi imefuta deni ya Somalia katika makubaliano yaliyokamilishwa kando ya mkutano wa marais wa Afrika na Urusi huko St Petersburg.

"Hatua hii itakuwa na jukumu kubwa katika kukamilika kwa mchakato wa kusamehewa madeni nchini," Waziri wa Fedha wa Somalia Bihi Egeh alisema kuhusu mpango huo na Moscow katika chapisho kwenye ukurasa wa Facebook wa wizara hiyo.

Mkataba uliotiwa saini Jumatano kati ya Egeh na naibu waziri wa fedha wa Urusi Timur Maksimov ulihusu mikopo ya Klabu ya Paris, Naibu Waziri Mkuu wa Somalia Salah Ahmed Jama aliambia shirika la habari la Urusi RIA Novosti.

Huku ikijwamua kutoka kw achangamoto ya vita ya muda mrefu, Somalia inatafuta kupata msamaha mkubwa wa deni la nje chini ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Mpango wa Benki ya Dunia wa Nchi Maskini Wenye Madeni Kubwa (HIPC).

Jamaa aliongeza kuwa, chini ya makubaliano hayo, sehemu ya deni hilo itafutwa mara moja huku sehemu ikitakiwa kupangiwa ratiba ya malipo.

Makubaliano hayo na Somalia yanakuja wakati rais wa Urusi Vladimir Putin anataka kutumia vyema mkutano wa viongozi wa Afrika huko St Petersburg, ili kuimarisha uhusiano na mataifa ya Afrika, na kurudisha nyuma juhudi za Magharibi za kuitenga Moscow kutokana na uvamizi wake nchini Ukraine.

TRT Afrika