Wanaume wanne wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya watu 137 katika jumba la tamasha la Moscow waliwekwa rumande, huku Urusi ikiadhimisha siku ya kitaifa ya maombolezo kufuatia shambulio lililodaiwa na kundi la kigaidi la Daesh.
Washukiwa wote wanne wameshtakiwa kwa ugaidi, kulingana na mahakama ya wilaya ya Basmanny ya Moscow, na wanakabiliwa na kifungo cha maisha. Kuzuiliwa kwao kumewekwa hadi Mei 22 lakini kunaweza kuongezwa kulingana na tarehe ya kesi yao.
Mahakama ilisema washtakiwa wawili walikiri hatia, na mmoja wao, kutoka Tajikistan, "alikubali hatia yake kabisa".
Rais Vladimir Putin ameapa kuwaadhibu wale waliohusika na "shambulio la kigaidi la kinyama", na Jumamosi alisema watu hao wanne wenye silaha walikamatwa walipokuwa wakijaribu kukimbilia Ukraine. Kiev imekanusha vikali uhusiano wowote na shambulio hilo.
Putin hajazungumzia madai ya kundi la Daesh kuhusika.
Takriban watu 137, wakiwemo watoto watatu, waliuawa Ijumaa jioni wakati watu wenye silaha walipovamia Jumba la Jiji la Crocus katika kitongoji cha kaskazini mwa Moscow cha Krasnogorsk kisha kuchoma moto jengo hilo.
Ni shambulio baya zaidi barani Ulaya kuwahi kudaiwa na Daesh.
Kamati ya Uchunguzi ya Urusi ilichapisha video ya washukiwa hao wanne wakiburutwa hadi katika makao yake makuu mjini Moscow.
Hakukuwa na taarifa yoyote kuhusu washukiwa wengine saba waliokamatwa kuhusiana na shambulio hilo.
Maafisa wamesema watu hao wenye silaha walikuwa raia wa kigeni.
'Bunduki za rashasha, visu, mabomu ya moto'
Kundi la Daesh lilichapisha Jumamosi kwenye Telegram kwamba shambulio hilo "lilitekelezwa na wapiganaji wanne wa Daesh waliokuwa na bunduki, bastola, visu na mabomu ya moto" kama sehemu ya "vita vikali" na "nchi zinazopigana na Uislamu".
Video inayodumu kwa takriban dakika moja na nusu, ambayo inaonekana ilirekodiwa na watu wenye silaha, imechapishwa kwenye akaunti za mitandao ya kijamii ambazo kwa kawaida hutumiwa na Daesh, kulingana na kundi la kijasusi la SITE
Video hiyo - ambayo inaonekana kurekodiwa kutoka kwa ukumbi wa tamasha - inaonyesha watu kadhaa walioficha nyuso zao na sauti wakifyatua risasi huku maiti zimetapakaa sakafuni na moto ukianzia nyuma.
Wachunguzi wa Urusi walisema kwamba baada ya kupita katika jumba hilo la maonyesho wakiwafyatulia risasi watazamaji hao, watu hao wenye silaha walilichoma moto jengo hilo na kuwanasa wengi ndani.
Maafisa wa afya walisema idadi ya waliojeruhiwa imeongezeka hadi 182, na watu 101 bado wako hospitalini, ambapo 40 walikuwa katika hali "mbaya" au "mahututi sana".
Shambulio hilo lilikuwa baya zaidi nchini Urusi tangu kuzingirwa kwa shule ya Beslan mnamo 2004.
Wizara ya hali ya dharura kufikia sasa imewataja 29 kati ya waathiriwa, lakini moto huo umefanya kuwa mgumu mchakato wa kuwatambua.
Wizara siku ya Jumapili ilichapisha video ya vifaa vizito vikiwasili katika ukumbi huo ili kubomoa miundo iliyoharibika na kuondoa vifusi.
Kuvunjika moyo
Katika mitaa ya mji mkuu siku ya Jumapili, kulikuwa na mshtuko na huzuni.
"Ni janga. Nilivunjika moyo kikweli," Ruslana Baranovskaya, 35, aliiambia AFP.
"Watu hawatabasamu... kila mtu anahisi hasara," alisema Valentina Karenina mwenye umri wa miaka 73, mstaafu aliyesimama kwenye barabara karibu na Red Square.
Makumbusho, na sinema kote nchini zilifungwa na mabango yalibadilishwa na mabango ya ukumbusho.
Waombolezaji waliendelea kumiminika kwenye ukumbi wa tamasha kaskazini-magharibi mwa Moscow kuweka maua kama heshima kwa waathiriwa.
Zaidi ya watu 5,000 walichangia damu kufuatia shambulio hilo, maafisa walisema, huku wengi wakiwa wamesimama kwenye foleni ndefu nje ya kliniki.
Nje ya nchi, watu waliweka maua za rambirambi nje ya balozi za Urusi kwa huruma.
Putin siku ya Jumamosi aliapa "kulipiza kisasi na kufany amaangamizi " kwa "magaidi, wauaji na wasio binadamu" waliotekeleza "shambulio la kigaidi la kinyama".
Washirika wake kadhaa wametoa wito kwa nchi hiyo kuondoa kusitishwa kwa hukumu ya kifo, na hivyo kuzua wasiwasi miongoni mwa wakosoaji wa Kremlin.
Putin ailaumu Ukrain
Taarifa ya Putin Jumamosi ilidokeza kuhusika kwa Ukraine.
"Walijaribu kutoroka na walikuwa wakisafiri kuelekea Ukraine, ambapo, kwa mujibu wa data za awali, dirisha lilitayarishwa kwa ajili yao upande wa Ukraine kuvuka mpaka wa jimbo," Putin alisema kuhusu washambuliaji hao katika hotuba yake ya televisheni.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, katika hotuba yake ya jioni Jumamosi, alikataa pendekezo lolote kwamba Kiev ilihusika.
Washington pia ilitupilia mbali pendekezo lolote kwamba Kiev imehusika