Ujerumani imeelezea wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa ubaguzi dhidi ya Waislamu nchini humo tangu kuanza kwa vita vya Gaza mnamo Oktoba 7.
Mashambulizi yoyote dhidi ya Waislamu nchini Ujerumani, kwa sababu za kidini au nyinginezo, "hayakubaliki kabisa," msemaji wa serikali Steffen Hebestreit alisema katika mkutano na waandishi wa habari mjini Berlin siku ya Jumatatu.
"Takriban Waislamu milioni 5 nchini Ujerumani wana kila haki ya kulindwa," aliongeza.
Wiki iliyopita, Muungano wa 'Alliance Against Islamophobia and Anti-Muslim Hate (CLAIM)' inayotetea waislamu, yenye makao yake makuu mjini Berlin, ulionya juu ya kuongezeka kwa ubaguzi dhidi ya Waislamu wakati wa mzozo unaozidi kuongezeka kati ya Israel na Palestina huko Gaza.
"Tunashuhudia kukithiri kwa ubaguzi dhidi ya Waislamu nchini Ujerumani. Hili ni jambo ambalo sote tunapaswa kuwa na wasiwasi nalo na linahitaji kuchukuliwa kwa uzito,” alisema Rima Hanano, mkuu wa shirika lisilo la kiserikali.
"Lazima tusiruhusu misimamo isiyo ya kibinadamu kurekebishwa zaidi na hivyo kuhatarisha mshikamano wa kijamii. Watu wote lazima walindwe dhidi ya unyanyasaji wa ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya Wayahudi na unyanyasaji mwingine wa kinyama na vitisho,” aliongeza.
Mashambulzi ya mitandawo ya kijamii
CLAIM imeripoti visa 53 vya vitisho dhidi ya Waislamu, ghasia na ubaguzi katika muda wa wiki mbili na nusu pekee zilizopita, ikiwa ni pamoja na mashambulizi 10 kwenye misikiti.
Huenda ikawa kuna idadi kubwa ya matukio dhidi ya Waislamu ambayo hayajaripotiwa au kurekodiwa, kwa mfano, hii inatumika pia kwa matamshi ya chuki dhidi ya Uislamu kwenye mitandao ya kijamii.
CLAIM ilitoa wito wa kuchukuliwa hatua madhubuti za kukabiliana na ubaguzi wa rangi dhidi ya Waislamu na kuwalinda walioathirika.
"Kupambana na ubaguzi wa rangi dhidi ya Waislamu, chuki dhidi ya Wayahudi na itikadi nyingine potofu ni muhimu zaidi kuliko hapo awali kwa demokrasia yetu na mshikamano wa jamii. Haja ya kuchukuliwa hatua ni kubwa,” kulingana na NGO.