Mtandao wa video fupi wa TikTok imejitetea kuwa imechukua hatua mara moja ikiwemo kuhamasisha rasilimali na wafanyikazi ili kukabiliana na chuki na habari potofu zilizogubika mgogoro wa Palestina na Israeli.
Siku ya alhamisi, mkuu wa viwanda wa Umoja wa Ulaya - EU, Thierry Breton alitoa saa 24 kwa tik tok ili kufafanua hatua za kina zilizochukuliwa ili kukabiliana na kuenea kwa habari potofu zinazohusiana na mzozo wa Mashariki ya kati huku pia akifungua uchunguzi dhidi ya mtandao wa Elon Musk wa X.
Kupitia taarifa yake, Tik Tok iliorodhesha hatua ilizochukua, ingawa ilikataa kusema jinsi ilivyokuwa imemjibu Breton.
"TikTok inapinga vikali ugaidi. Tunashtushwa na vitendo vya kutisha vya ugaidi nchini Israeli wiki iliyopita. Pia, tumehuzunishwa sana na mzozo wa kibinadamu unaozidi kuongezeka huko Gaza, " TikTok ilisema.
TikTok, inayomilikiwa na kampuni ya Kichina ya ByteDance, ilisema kuwa hatua zake ni pamoja na kuzindua kituo cha amri, kuimarisha mifumo yake ya kugundua kiotomatiki ili kuondoa yaliyomo kwenye picha na vurugu na kuongeza wasimamizi zaidi wanaozungumza kiarabu na kiebrania.
Vilevile, ilikuwa ikiondoa maudhui ambayo yanashambulia au kuwadhihaki waathiriwa wa vurugu au kuchochea vurugu.
Pia, ilikuwa imeongeza vizuizi juu ya ustahiki wa huduma yake ya matangazo ya moja kwa moja na ilikuwa ikishirikiana na mashirika ya utekelezaji wa sheria pamoja na wataalam wengine.