Sudan Kusini: Rais Salva Kiir awasili Misri kukutana na Rais Sisi

Sudan Kusini: Rais Salva Kiir awasili Misri kukutana na Rais Sisi

Rais Salva Kiir anatarajiwa kujadili hali ya Sudan na mwenyeji wake Rais Sisi
Rais Salva Kiir anatarajiwa kujadili hali ya Sudan na mwenyeji wake Rais Sisi. Picha: Ikulu Sudan Kusini

Ziara ya rais Salva Kiir mjini Misri inajiri takriban miezi sita tangu rais huyo na viongozi kadhaa wa kanda kukutana Cairo mnamo Julai 2023, kuhudhuria mkutano wa majirani wa Sudan uliojulikana kama "kuendeleza mifumo madhubuti" ya utatuzi wa hali ya amani nchini Sudan kupitia juhudi za kikanda na kimataifa.

Mkutano huo, ulioongozwa na rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi, uliwavutia wawakilishi kutoka nchi saba ambazo zinapakana na Sudan, ikiwemo Sudan Kusini, Misri, Chad, Eritrea, Ethiopia, Libya na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR).

"Ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano kati ya Juba na Cairo katika nyanja mbalimbali, pamoja na majadiliano juu ya masuala ya kikanda na kimataifa." Ikulu ya rais Sudan Kusini ilisema.

Aidha, vyombo vya habari vya Sudan yamemnukuu Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan Kusini, James Pitia Morgan akisema kuwa "masuala mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vita vya Sudan yatajadiliwa."

Aidha, itakumbukwa kuwa mkataba wa amani wa Juba ulisainiwa huko Juba chini ya uangalizi wa rais Kiir mnamo Oktoba 3, 2020, kati ya Serikali ya Sudan na watia saini 14. Chad, huku falme za Kiarabu na IGAD zikiwa wadhamini, nazo Misri na Qatar wakiwa ni mashahidi wa makubaliano ya amani.

Mwezi uliopita, pande zinazozozana nchini Sudan zimerejea tena mazungumzo mjini Jeddah, Saudi Arabia kufuatia mwaliko wa Marekani na Saudi Arabia kwa lengo la kumaliza mvutano huo ambao umeendelea kwa zaidi ya miezi sita na kupelekea mauaji ya maelfu ya watu.

Mazungumzo ya upatanishi ya hivi karibuni yanafanyika "chini ya ushirikiano" na mwakilishi wa Umoja wa Afrika na Mamlaka ya Serikali za Maendeleo (IGAD).

Kwa upande wake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Kuwait imesema kwenye X kwamba "Uvamizi wa Israeli na uchokozi wake dhidi ya watu wa Palestina umefikia hatua hatari na kiburi chake kimefikia kiwango cha ukatili ambacho hakijawahi kutokea katika historia ya wanadamu.”

AA