Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza kwamba, ni magari machache tu ya mizigo ndio yataruhusiwa kuvuka mpaka wa Rafah kutoka Misri kuingia Gaza kuanzia Ijumaa.
Misri pia imethibitisha hilo huku mamia ya magari ya mizigo yakisubiri katika lango kuu la Gaza ambalo limeshambuliwa na Israel.
“Rais wa Misri Abdel Fattah al Sisi na mwenzake wa Marekani Joe Biden wamekubalaino muendelezo wa kufikishwa kwa misaada ya kibinadamu Gaza kupitia kituo cha Rafah," amesema msemaji wa rais wa Misri Ahmed Fahmy katika taarifa yake bila kutaja tarehe maalumu.
Israel, ambayo inaendesha mpaka wa Rafah kutoka upande wa Palestine, kwa upande wake imesema siku ya Jumatano kwamba imetoa ishara ya kuruhusu idadi maalumu ya misaada ya kibinadamu kuingia Gaza.
Msaada muhimu kufika Gaza kutokana na makubaliano mapya,