Papa Francis alianza ziara yake nchini Mongolia kwa kuangazia uhifadhi wa mazingira ambayo alisema, nchi hiyo imeathirika pakubwa na mabadiliko ya tabia nchi.
Katika hotuba yake, Francis pia alizungumzia vitisho kwa mazingira, akisema mila ya asili ya Wamongolia ya kuhamahama inaheshimu usawa wa asili lakini kwamba leo kuna haja ya "kupambana na athari za uharibifu wa binadamu" wa mazingira.
Mongolia ni moja wapo ya nchi zilizoathiriwa zaidi na mzozo wa hali ya hewa, na wastani wa joto kuongezeka kwa zaidi ya nyuzi 2 Celsius tangu 1940.
Papa huyo alisema kuwa tatizo la mabadiliko ya tabia nchi limeenea kote ulimwenguni na kufikia kiwango cha hatari.
''Mabadiliko ya tabia nchi sasa limejuwa jambo la dharura na haliwezi kuahirishwa tena,'' alisema Papa Francis.
Amani duniani
Papa wa Katoliki pia alizungumzi asuala la amani duniani akisema kuwa anakuja kama ''Hujaji wa amani anayefika kwa haraka.''
Papa Francis ametoa wito kwa viongozi kuondoa "wingu jeusi la vita," akizungumza katika nchi ambayo iko kati ya mataifa mawili yenye nguvu duniani - Urusi na Uchina - ambayo amelenga katika juhudi za kidiplomasia za Vatican juu ya Ukraine.
"Naoba mbingu zitusikie na kutufaidi leo, katika dunia hii iliyoharibiwa na migogoro isiyohesabika, kuwe na upya, kuheshimu sheria za kimataifa," alisema.
"Na mawingu meusi ya vita yaondolewe, yafagiliwe mbali na nia thabiti ya udugu wa ulimwengu mzima ambamo mivutano inatatuliwa kwa kukutana na mazungumzo, na haki za kimsingi za watu wote zimehakikishwa," alisema.
Kusudi ya ziara yake hii lilikuwa kutembelea jumuiya ndogo ya Wakatoliki ya Mongolia, ambayo ina wanachama 1,450 na ni mojawapo ya ndogo zaidi duniani.