Papa Francis anataka uchunguzi ufanyike ili kubaini iwapo mauaji ya halaiki yanafanyika huko Gaza, shirika la habari la Vatican liliripoti Jumapili.
"Kulingana na baadhi ya wataalam, kinachotokea Gaza kina sifa ya mauaji ya halaiki. Inapaswa kuchunguzwa kwa makini ili kubaini kama kinalingana na ufafanuzi wa kitaaluma uliotungwa na wanasheria na mashirika ya kimataifa," alisema katika kifungu cha kitabu chake kipya katika sehemu ya mahojiano, ''Hope Never Diappoints: Pilgrims Towards a Better World'', ambacho kinatarajiwa kutolewa Jumanne hii.
"Ninwafikiria wale wote wanaoondoka Gaza huku kukiwa na njaa ambayo imewakumba kaka na dada zao wa Kipalestina kutokana na ugumu wa kupata chakula na misaada katika eneo lao," Papa aliongeza, akimaanisha vikwazo vya Israeli ambavyo vinaruhusu msaada kidogo tu iklinganishwa na msaada unaohitajika na zaidi ya watu milioni 2 katika eneo lililozingirwa.
Israel imeendelea na mashambulizi makali dhidi ya Gaza tangu Oktoba 7, 2023, na kuua karibu Wapalestina 44,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na kufanya eneo hilo kuwa sehemu ambayo watu hawawezi kuishi.
Pia inakabiliwa na kesi ya mauaji ya halaiki katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki kwa hatua zake katika eneo lililozuiliwa kuingia misaada.