Marufuku hiyo dhidi ya mtandao wa X, ambayo ilianza kutekelezwa Jumamosi, inaifanya Brazil kujiunga na orodha ya nchi ambazo zimechukua hatua sawa dhidi ya mtandao wa kijamii.
Mbali na marufuku ya kudumu, baadhi ya mataifa yamezuia kwa muda ufikiaji wa X, ambayo zamani ilikuwa Twitter, ambayo mara nyingi imekuwa ikitumiwa na wapinzani wa kisiasa kuwasiliana.
Mataifa haya yamejumuisha Misri mwaka 2011 wakati wa ghasia za Arab Spring, Uturuki mwaka 2014 na 2023, na Uzbekistan karibu na uchaguzi wa rais wa 2021 wa nchi hiyo.
Hii hapa ni orodha ya baadhi ya nchi zingine zilizopiga mtandao wa X marufku.
China
Beijing ilipiga marufuku Twitter mnamo Juni 2009 - kabla ya mtandao huo kupata umaarufu katika vyombo vya habari vya Magharibi na siasa kwa muda mrefu wa 2010.
Kizuizi hicho kilikuja siku mbili kabla ya maadhimisho ya miaka 20 ya serikali kukandamiza maandamano ya kuunga mkono demokrasia katika uwanja wa Tiananmen wa mji mkuu.
Tangu wakati huo, watu wengi wa China wamegeukia njia mbadala na kutumia mitandao ya nyumbani kama vile Weibo na WeChat.
Iran
Twitter pia ilizuiwa Iran mwaka 2009, wakati wimbi la maandamano lilipozuka kufuatia uchaguzi wa rais wa Juni uliopingwa.
Mtandao huo hata hivyo umetumika tangu wakati huo kupitisha habari kwa ulimwengu wa nje kuhusu harakati za wapinzani.
Turkmenistan
Nchi iliyotengwa ya Asia ya Kati Turkmenistan ilizuia Twitter mapema miaka ya 2010 pamoja na huduma na tovuti nyingi za kigeni za mtandaoni.
Mamlaka huko Ashgabat hufuatilia kwa karibu matumizi ya wananchi ya mtandao, yanayotolewa kupitia kampuni ya serikali inayomiliki ukiritimba wa TurkmenTelecom.
Korea Kaskazini
Pyongyang ilifungua akaunti yake ya Twitter mwaka wa 2010 kwa nia ya kuwavutia wageni wanaopenda nchi hiyo.
Lakini mtandao huo Aprili 2016, ukapigwa marufuku pamoja na Facebook, YouTube na tovuti za kamari.
Ufikiaji wa mtandao zaidi ya tovuti chache za serikali uko chini ya uangalizi mkali wa serikali chini ya utawala wa Hermit, na ufikiaji unazuiwa kwa maafisa wachache wa vyeo vya juu.
Myanmar
Mtandao wa X imepigwa marufuku tangu Februari 2021, wakati mamlaka iligundua mtandao huo kutumiwa na wapinzani wa mapinduzi ya kijeshi yaliyopindua serikali ya kiraia ya Aung San Suu Kyi.
Tangu wakati huo, junta imekuwa ikizuia sana upatikanaji wa mtandao nchini Myanmar.
Urusi
Ufikiaji wa Twitter ulizuiliwa kutoka 2021 na Moscow, ambayo ililalamika kuwa tovuti hiyo ilikuwa ikiruhusu watumiaji kueneza "maudhui haramu."
Marufuku rasmi ilikuja Machi 2022, mara tu baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Watumiaji wengi wa Kirusi wanaendelea kuunganisha mtandao wa X kupitia huduma za VPN zinazowawezesha kuepuka kizuizi hicho.
Pakistani
Mtandao wa X umepigwa marufuku tangu kura za wabunge Februari mwaka huu.
Serikali ya Pakistan, ikiungwa mkono na jeshi, inasema kizuizi hicho ni kwa sababu za kiusalama.
Waziri mkuu wa zamani Imran Khan alilengwa na madai mengi ya udanganyifu yaliyoenezwa kupitia jukwaa dhidi ya chama chake cha upinzani.
Venezuela
Nicolas Maduro, ambaye alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa Julai licha ya tuhuma kubwa za udanganyifu, aliamuru ufikiaji wa X usitishwe kwa siku 10 mnamo Agosti 9 wakati vikosi vya usalama vilikuwa vikikabiliana maandamano yaliyoibuka nzima.
Hata hivyo marufuku bado inaendelea hata baada ya kumalizika kwa muda wa siku 10.
Brazili
Marufuku dhidi ya mtandao wa X imetoka kwa mahakama, kupitia jaji wa Mahakama ya Juu Alexandre de Moraes.
Sababu za marfuku hiyo ni uanzishaji upya wa akaunti ambazo zilikuwa zimeagizwa kusimamishwa na mahakama za Brazil.
Watumiaji wanaounganisha X kupitia VPN watatozwa faini ya reais 50,000 ($8,900) kwa siku.