twitter / Photo: AA

Huenda baadhi ya wasanii au watu wenye ushawishi mkubwa unaowafwatilia ni miongoni mwa walioporwa alama hiyo.

Papa Fransis, Christiano Ronaldo, Justine Bieber, Donald Trump na wengine wengi pamoja na kuwa na idadi kubwa ya wafuasi katika mtandao huo wameondolewa tiki ya bluu ya ishara ya kuidhinishwa katika kurasa zao.

Haya yanajiri saa chache baada ya mtandao huo wa kijamii kuondoa lebo "zinazohusishwa na serikali" na "zinazofadhiliwa na serikali" kutoka kwenye akaunti za vyombo vya habari, kulingana na mashirika ya habari mnamo Ijumaa.

Vyombo vingi vya habari kutoka mataifa ya Magharibi, Urusi, Uchina na nchi zingine ambazo hapo awali zilikuwa na lebo hizo hazikuonyeshwa tena, kulingana na shirika la habari la AFP.

Mmiliki Elon Musk, ambaye ameona uwekezaji wake wa dola bilioni 44 kwenye tovuti ukidorora, awali aliahidi kuondoa kile alichoeleza kama "mfumo wa mabwana na wakulima."

Badala yake alitangaza kuuza beji ya bluu kwa mtu yeyote ambaye angelipa $8 kwa mwezi, katika hatua aliyosema mwaka jana "itaweka demokrasia uandishi wa habari na kuwezesha sauti ya watu."

TRT Afrika