Mawaziri wa mambo ya nje wa Uturuki na Urusi wakutana mjini Moscow kwa mazungumzo

Mawaziri wa mambo ya nje wa Uturuki na Urusi wakutana mjini Moscow kwa mazungumzo

Mevlut Cavusoglu, Sergey Lavrov wafanya mkutano wa faragha kando ya mkutano wa pande nne kuhusu Syria
FM ministerial meeting / Photo: AA

Mawaziri wa mambo ya nje wa Uturuki na Urusi wamekutana kwa mazungumzo mjini Moscow siku ya Jumatano.

Mevlut Cavusoglu na Sergey Lavrov wamefanya mkutano wa faragha kando ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje kati ya Uturuki, Urusi, Iran na serikali ya Syria.

Katika mkutano huo wa pande nne, mawaziri hao wanatarajiwa kubadilishana mawazo kuhusu kuhalalisha uhusiano wa Uturuki na Syria.

Pia wanapanga kujadili kukabiliana na ugaidi, mchakato wa kisiasa wa kumaliza vita nchini Syria, na masuala ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na kurejea kwa hiari, salama na kwa heshima kwa Wasyria ambao waliiacha nchi yao kutokana na vita.

Desemba iliyopita, mawaziri wa ulinzi na wakuu wa kijasusi kutoka Uturuki, Urusi, na utawala wa Syria walikutana mjini Moscow na kukubaliana kuendelea na mikutano ya pande tatu ili kuhakikisha utulivu nchini Syria na eneo zima.

Iran pia ilijumuishwa katika mazungumzo hayo, huku Uturuki awali ikisema kwamba Ankara "itafurahishwa ikiwa Iran itahusika katika mchakato huu."

Syria imekumbwa na vita vikali vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwanzoni mwa 2011 wakati utawala wa Assad ulipo dhibiti maandamano ya kuunga mkono demokrasia kwa ukatili usio tarajiwa.

AA