Afrika Kusini iliweka orodha ya madai ya mauaji ya halaiki yaliyofanywa na Israel/ picha Kutoka International Court of Justice

Tarehe 11 na 12 Januari mwaka huu, Afrika Kusini iliishtaki Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ.

Afrika Kusini iliweka orodha ya madai ya mauaji ya halaiki yaliyofanywa na Israel katika siku ya kwanza ya kusikilizwa kwa kesi hiyo Alhamisi, huku Israel ikijitetea Ijumaa.

"Mahakama sasa itaanza mashauri yake," ICJ imesema katika taarifa,

Madai ya Afrika Kusini mbele ya Mahakama

Kulingana na Mahakama ya ICJ haya ndiyo yaliyowakilishwa na Afrika Kusini:

  • Taifa la Israel lisitishe mara moja operesheni zake za kijeshi ndani na dhidi ya Gaza
  • Taifa la Israeli lihakikishe kwamba vikosi vyovyote vya kijeshi au visivyo vya kawaida vinavyoweza kuelekezwa, kuungwa mkono au kuathiriwa nayo, pamoja na mashirika na watu wowote ambayo inaweza kuwa chini ya udhibiti wake, zisichukue hatua ya kuendeleza operesheni za kijeshi .
  • Israel iwache kuwaua Wapalestina
  • Israel iwache kusababisha madhara makubwa ya mwili au kiakili kwa washiriki wa kikundi
  • Israel iwache kufanya kwa makusudi kuathiri hali ya maisha ya Wapalestina na uharibifu wake wa kimwili kwa ujumla
  • Israel iwache kuweka hatua zinazokusudiwa kuzuia Wapalestina kuzaa zaidi
  • Israel iwache kuwafukuza na kuwalazimisha Wapalestina kutoka kwenye makazi yao.
  • Israel ihakikishe upatikanaji wa chakula na maji ya kutosha na upatikanaji wa misaada ya kibinadamu, ikiwa ni pamoja na kupata mafuta ya kutosha, malazi, nguo, usafi na usafi wa mazingira

Madai ya Israel mbele ya Mahakama

  • Israel ilikataa ombi hatua za muda zilizowasilishwa na Kusini Afrika

  • Israel imeitaka mahakama kuondoa kesi kutoka kwa orodha yake ya jumla

  • " Uamuzi wa Mahakama utatolewa katika mkutano wa hadhara, ambao tarehe yake itatangazwa kwa wakati wake." Mahakama ya ICJ imesema katika taarifa hiyo.

TRT Afrika