Korea Kusini kupunguza jinsi yakupima umri ya watu | Picha: TRT Afrika

Kuanzia Julai 2023, umri ulioripotiwa kwenye hati yoyote rasmi lazima uhesabiwe kwa mujibu wa mbinu ya kimataifa .

Hii juhudi za nchi hiyo kupunguza mkanganyiko kati ya mbinu mbalimbali za nchi hiyo za kuhesabu umri.

Hivi sasa nchini Korea Kusini, kuna njia nyingi za kuhesabu umri.

Njia maarufu zaidi ni "umri wa Kikorea," ambapo mtoto huchukuliwa kuwa mwenye umri wa mwaka anapozaliwa kwa imani kuwa maisha huanza tumboni. Na mnamo Januari 1, kila mtu nchini hutimiza mwaka mwingine zaidi.

Njia nyingine ni "kuhesabu umri" ambayo umri wa mtu huanzia sifuri wakati wa kuzaliwa na mwaka mmoja huongezwa kila mwanzo wa Mwaka Mpya.

Nyingine ni mfumo wa "umri wa kimataifa," ambao Korea Kusini inaupitisha sasa, kuhesabu huanzia sifuri na huongeza mwaka mmoja kila mwaka katika siku ya kuzaliwa ya mtu binafsi.

Kwa hivyo, kwa mfano, ikiwa mtu amezaliwa mnamo Desemba 10, 2000, atakuwa na umri wa miaka 22 kwa umri wa kimataifa, 23 kwa umri wa kuhesabu na 24 kwa umri wa Korea.

"Marekebisho hayo yanalenga kupunguza gharama zisizo za lazima za kijamii na kiuchumi, kwa sababu migogoro ya kisheria na kijamii pamoja na mkanganyiko unaendelea kutokana na njia tofauti za kuhesabu umri," alisema Yoo Sang-bum wa chama tawala cha People Power Party bungeni.

Kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari, idadi kubwa ya Wakorea wako tayari kutumia umri wao wa kimataifa ili kupunguza mkanganyiko wa umri nchini humo.

Asilimia 86.2 ya waliohojiwa walijibu kuwa watatumia umri wa Kimataifa katika maisha yao ya kila siku.

Waziri mmoja alisema mabadiliko hayo yatakuwa mazuri kwa mawazo ya raia wengi wa Korea.

"Ikiwa watu wanahisi umri wao umepunguzwa kwa mwaka mmoja au miwili, itakuwa na matokeo mazuri kwa jamii, tutashirikiana kuitangaza kwa umma " alisema Waziri Lee Wan-kyu wa Wizara ya Sheria za Serikali.

Hatua hiyo pia ni baadhi ya ahadi ya serikali ya sasa ya kampeni ya kupitisha mfumo wa kuhesabu umri ambao ulimwengu kwa jumla unatumia.

Yaliyomo katika ahadi ya kutatua kero za wananchi kwa kuweka kiwango cha umoja yametekelezwa katika takriban miezi sita baada ya kuapishwa kwa serikali,” Waziri wa Sheria Han Dong-hoon alisema.

Reuters