Rais wa Marekani Joe Biden amesema mauaji ya kiongozi wa kikundi cha Kipalestina cha Hamas Ismail Haniyeh hakijsaidia kumaliza vita vya Israeli dhidi ya Gaza.
Kumekuwa na hatari ya kuongezeka kwa vita vya Mashariki ya Kati baada ya mauaji ya Haniyeh nchini Iran yalisababisha vitisho vya kulipiza kisasi dhidi ya Israeli.
Kikundi cha Hamas na kile cha kimapinduzi vilithibitisha kifo cha Haniyeh, ambaye alishiriki kwenye mazungumzo ya kumaliza vita katika eneo la Gaza.
"Hayatosaidia lolote," Biden aliwaambia wanahabari baada ya kuulizwa iwapo mauaji ya Haniyeh yatazorotesha mazungumzo ya amani.
Biden pia alisema alikuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu mapema Alhamisi.
TRT Afrika