Erdogan alihakikisha kwamba Türkiye atasalia pamoja na marafiki wote wanaopigania kwa dhati mfumo wa haki wa kimataifa na UNSC inayoakisi hali halisi ya dunia ya leo. / Picha: AA

Muundo wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo kwa sasa liko mbali na kutekeleza wajibu wake wa kuhakikisha amani na usalama wa dunia, "lazima ubadilishwe kwa kiasi kikubwa," Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema.

"Kabla vita havijaimeza dunia yetu zaidi, kabla watu na jamii zaidi hawajateseka, na kabla damu zaidi ya wasio na hatia haijamwagika, muundo wa Baraza la Usalama la UN, ambalo kwa sasa liko mbali na kutekeleza wajibu wake wa kuhakikisha amani na usalama wa dunia, lazima ubadilishwe kwa kiasi kikubwa. Haya ndio matarajio ya ubinadamu kutoka kwetu," Erdogan alisema kwenye X siku ya Jumatano.

Akionyesha msimamo wa Uturuki, Erdogan alirudia, "Tutaendelea kusema, 'Dunia ni kubwa kuliko nchi tano,' na tutatenda kwa uelewa kwamba 'Dunia yenye haki zaidi inawezekana.'"

Erdogan alihakikisha kwamba Uturuki itaendelea kusimama pamoja na marafiki wote wanaojitahidi kwa dhati kwa mfumo wa kimataifa wenye haki na Baraza la Usalama la UN linaloakisi hali halisi ya dunia ya leo.

Ukosefu wa uwakilishi wa kudumu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres pia alisisitiza umuhimu wa nafasi ya Afrika katika amani na usalama wa dunia siku ya Jumatano, akisema kwamba ukosefu wa uwakilishi wa kudumu katika Baraza la Usalama la UN (UNSC) ni "haikubaliki."

Akisisitiza haja ya haraka ya mageuzi yanayojumuisha Afrika katika uwakilishi wa Baraza, Guterres alisema kwenye X, "Baraza la Usalama lilibuniwa na washindi wa Vita vya Dunia vya Pili. Dunia imebadilika lakini muundo wa Baraza haujaendana na kasi hiyo."

"Hatuwezi kukubali kwamba hakuna mwanachama wa kudumu anayewakilisha Afrika - bara lenye watu zaidi ya bilioni moja. Sauti za Waafrika, ufahamu na ushiriki lazima viletwe katika majadiliano na hatua za Baraza."

Erdogan alisisitiza umuhimu wa Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres kuelezea kwa uwazi na kwa dhati maoni yake kuhusu kufanyia mageuzi UNSC kwa njia iliyo haki na inayoendana na hali ya sasa ya dunia.

Rais wa Uturuki pia aliongeza kwamba bara la Afrika na mataifa yote ya Kiafrika yanapaswa kupewa fursa ya kuchangia katika mfumo huu wa haki.

TRT World