Mwanajeshi wa Uturuki amefariki baada ya kujeruhiwa katika shambulizi la kigaidi katika eneo la operesheni ya kupambana na ugaidi la Uturuki kaskazini mwa Iraq, kulingana na Wizara ya Ulinzi ya Kitaifa ya Uturuki.
Mwanajeshi huyo, Erkan Selcuk, aliyejeruhiwa Ijumaa, alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata kutokana na mlipuko wa kilipuzi kilichowekwa na magaidi wa PKK kwenye eneo la Operesheni Claw-Lock ya Uturuki.
Baadaye alifariki hospitalini.
Wizara hiyo ilituma salamu za rambirambi kwa familia ya Selcuk, Jeshi la Uturuki na taifa.
Kundi la kigaidi la PKK limejulikana kuwa linaendeleza shughuli zake katika eneo hilo.
Uturuki ilizindua Operesheni Claw-Lock mwezi Aprili 2022 ili kulenga maficho ya kundi la kigaidi la PKK katika maeneo ya Metina, Zap na Avasin-Basyan kaskazini mwa Iraq, yaliyo karibu na mpaka wa Uturuki.
Katika kampeni yake ya zaidi ya miaka 35 ya ugaidi dhidi ya Uturuki, PKK -- iliyoorodheshwa kama shirika la kigaidi na Uturuki , Marekani na EU - imehusika na vifo vya zaidi ya watu 40,000, ikiwa ni pamoja na wanawake,na watoto.